Posts

Showing posts from November 11, 2018

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

Image
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0654-105503 0692-794942                               SEHEMU YA 1      Ilikuwa ni siku ya jumatano naelekea msamvu kituo cha mabasi kwenda kumpokea mgeni ambaye ni mtoto wa shangazi. Kiukweli sikuwa namfahamu kisura japo nilikuwa nalijua jina lake tu, kwasababu mama alikuwa akiniambia story za kumuhusu huyo binamu yangu.     Nilipofika msamvu kituo cha mabasi sikujua wapi pakuanzia, kwasababu mtu niliemfuata sikuijua sura yake na ukizingatia kwa wakati huo hapakuwa na simu za mkononi. Wakati nikiwa nimesimama huku nimeduwaa, ghafla likaingia basi la Abood pale kituoni likitokea dar es salaam, nililisindikiza kwa macho lile basi mpaka sehemu lilipo simama. Taratibu nilianza kujongea kulifuata lile basi nikidhania niliyefuata labda atakuwa ndani mwa lile basi. Nilipokaribia kufika, moyo ulisita kuendelea kulifuata lile basi ...