MALIPO YA USALITI

MALIPO YA USALITI By Theostar Kwa mawasiliano zaidi 0673779766 0782589866 SEHEMU YA 1 Juma na Hairath ni wapenzi wanaopendana sana. Mahusiano yao ya kimapenzi yamedumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu bila kuoana. Juma alikua ni mfanyakazi katika hoteli ya Cate Hotel inayopatikana Kingorwilwa mjini Morogoro. Kitengo chake cha kazi kilikua cha kupokea wageni mbalimbali wanaofika katika hoteli hio. Siku moja Juma akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi alitembelewa na mgeni aliyekuwa anafahamiana nae. "Karibu Halieth" (sauti ya Juma ilisikika kumkaribisha mgeni aliyeingia muda huo)... Asante! (mgeni "Halieth" alishukuru baada ya kukaribishwa na kukaa kwenye kiti kimojawapo vilivyoandaliwa kwa ajili ya wageni wanao ingia hotelini hapo, kisha akaendelea kuongea), habari za kazi rafiki yangu.. Mungu anasaidia vema, kazi zinaenda vizuri, sijui kwa upande wako...