MALIPO YA USALITI

                   

MALIPO YA USALITI
By Theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0673779766
0782589866

                SEHEMU YA 1

  Juma na Hairath ni wapenzi wanaopendana sana. Mahusiano yao ya kimapenzi yamedumu kwa muda wa mwaka mmoja na nusu bila kuoana.

  Juma alikua ni mfanyakazi katika hoteli ya Cate Hotel inayopatikana Kingorwilwa mjini Morogoro. Kitengo chake cha kazi kilikua cha kupokea wageni mbalimbali wanaofika katika hoteli hio.

Siku moja Juma akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi alitembelewa na mgeni aliyekuwa anafahamiana nae. "Karibu Halieth" (sauti ya Juma ilisikika kumkaribisha mgeni aliyeingia muda huo)...

Asante! (mgeni "Halieth" alishukuru baada ya kukaribishwa na kukaa kwenye kiti kimojawapo vilivyoandaliwa kwa ajili ya wageni wanao ingia hotelini hapo, kisha akaendelea kuongea), habari za kazi rafiki yangu..

Mungu anasaidia vema, kazi zinaenda vizuri, sijui kwa upande wako...

Kwangu pia namshukuru Mungu kazi zinaenda vizuri kabisa...

Kweli, hilo ni jambo la kumshukuru Mungu! Karibu sana (Juma alimkaribisha Halieth kwa mara nyingine kwa ajili ya kumuandaa aseme kile kilichompeleka mahala pale)... 

Asante! Nimekuja kukusalimia tu na kukuona maana siku mbili hizi hatujaonana na kila nilipopiga simu yako simu zilikua zinagoma kuingia nikawa natuma na ujumbe lakini ulikua unashindwa kuingia kwako, nikashindwa kujua tatizo nikaona bora nikutembelee kazini kwako nijue kinachokusibu...

Nashukuru sana kwa kunijali Halieth pia nikuombe samahani kwa kukutia presha. Laini yangu ilifungiwa kwa sababu sikuisajili kwa alama ya vidole, hii laini ninayoitumia hapa nimeazimwa na rafiki yangu nayo naitumia kwa muda tu...

Pole! Nimefurahi sana kukuona ukiwa salama maana nilikua na wasiwasi sana juu yako...

Nisamehe sana kwa kukutia wasiwasi jamani! Niandikie namba zako (Juma aliomba tena msamaha na kumpatia Halieth simu yake aingize namba zake)...

Mimi naondoka ila naomba badae tukapate chakula cha usiku pamoja (Halieth alimuaga Juma baada ya kumaliza kuingiza namba zake kwenye simu ya Juma na kumwalika wakawe pamoja kwenye chakula cha usiku)...

Sawa! Tutakutana wapi? (Juma aliukubari mwaliko na kumuuliza Halieth mahala pa makutano)...

Tukutane Suzy's restaurant mida ya saa mbili, nadhani patatufaa pale...

Sawa! Nitakujuza badae nikiwa tayari kuja...

Asante kwa kuukubari mwaliko wangu (Halieth alimshukuru Juma kwa kuubari mwaliko wake huku akionekana kuwa ni mwenye shauku kubwa ya kuwa pamoja na Juma usiku huo)...

Usijali Halieth, tutakuwa pamoja (Juma alimtoa wasiwasi Halieth baada ya kugundua kuwa alijawa na shauku)...

Haya! Ngoja nikuache uendelee na kazi (Halieth alisema hivyo huku akiwa anaituka toka kwenye kiti alichokuwa amekaa tayari kwa kuondaka)...

Poa!...

Kwaheri (Halieth aliaga na kutoka nje tayari kuianza safari)...

(Juma alimsindikiza Halieth kwa macho tu yaliyoyokuwa yamejawa na tamaa ya kutaka kumwona akiwa anatembea kwa jinsi anavyozichezesha nyama za makalio yake)............... ITAENDELEA

 

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.