PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                             
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503
    SEHEMU YA 3

    Ilipoishia sehemu ya pili (2)...... Tukiwa tunakunywa juisi mimi na Jenny, mama alisimama na kusema "ngoja nikuache mwanangu niandae chakula"...
"sawa aunty" (Jenny alijibu), mama alielekea jikoni tayari kuandaa chakula na kutuacha pale wenyewe tukiwa wawili tu............. SASA ENDELEA
     
     Kimya kilitawala kwa muda kidogo huku kila mmoja akiwa anausikilizia utamu wa ile juisi. "Daah juisi ni tamu aisee" (Jenny alianza kuongea na kuuvunja ukimya)....
"ni utaalamu wangu huo" (nilimjibu Jenny kwa kujisifu)....
"Mmmmmmh ujue kutengeneza juisi hivi, ulinge" (Jenny alinibeza)....
(nikacheka kidogo na kumuuliza) "kwahiyo Jenny huamini?"
"nitakuaminije mtu muongo kama wewe, huoni hata aibu unavyonidanganya, muone pale" (Jenny alinishushua)....
"haya, Kama unapingana na ukweli, lakini huo ndio ukweli wenyewe"....
"ngoja nije kumuuliza mama kama ni kweli"....
"aaaah mama atakudanganya maana atakwambia ndio yeye aliyetengeneza halafu siyo kweli"....
(Jenny alicheka kidogo na kusema) "nimekukamata na uongo wako"....
"hiii!, mimi siyo muongo heti, au kama huamini njoo umuulize mama basi" (mara nikasikia sauti ya mama ikiniita), "nakuja mama" (nikaitika uito wa mama).
   Nilisimama tayari kwenda kuitika wito. Nikiwa naelekea jikoni, Jenny alinisindikiza kwa macho mpaka nilipotokomea. "Nenda ukaandae meza mwanangu halafu ukimaliza uje uchukue chakula".... "sawa mama" (nilimjibu).
   Nilifanya kile nilichoelekezwa na mama, niliandaa sahani za chakula, vijiko pamoja na maji ya kunawa na ya kunywa. Baada ya kumaliza kuandaa meza, niliingia jikoni na kuchukua chakula na kukitenga mezani.
   "Jenny, twende tukale" (nilimuita Jenny na kumkaribisha chakula)....
"nenda ukale, mimi nimeshiba" (Jenny alinijibu)....
(nilimshangaa Jenny baada ya kunijibu vile na kumuuliza) "umekula nini Jenny kilichokushibisha wewe?"....
"yani juisi niliyokunywa hapa umenishibisha sitamani hata kula chochote"....
"mmmmmh!, Jenny acha utani basi"....
"siyo utani Theo, nakwambia ukweli ujue....
"poa, basi na mimi siendi kula.... (kimya kilitawala kwa muda mfupi kidogo huku tukiwa tumekaziana macho). Taratibu nilimsogelea Jenny pale alipokaa, nilimshika mikono yake "twende tukale Jenny na tukimaliza tu kuna zawadi nitakupa" (Jenny alitabasamu baada ya kusikia hivyo)................. ITAENDELEA 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI