PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. SEHEMU YA 4 Ilipoishia sehemu ya tatu (3)........ ( kimya kilitawala kwa muda mfupi kidogo huku tukiwa tumekaziana macho). Taratibu nilimsogelea Jenny pale alipokaa, nilimshika mikono yake "twende tukale Jenny na tukimaliza tu kuna zawadi nitakupa" (Jenny alitabasamu baada ya kusikia hivyo)............ SASA ENDELEA "Acha kunidanganya Theo, zawadi gani sasa utanipatia?".... "Aaaaah zawadi ni kitu cha siri, kwahiyo haitokuwa vizuri kuijua kabla ya wakati wake wa kuijua haujafika".... "sasa mimi si ndiyo mpokea zawadi!, kwahiyo napenda niijue kabla kama ni mbaya niikatae sasa hivi".... "weeeee, hilo ni bonge la zawadi!, utalipenda mwenyewe tu, ila sikwambii kuwa ni zawadi gani mpaka tukale kwanza tushibe...