PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                           
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
SEHEMU YA  4

   Ilipoishia sehemu ya tatu (3)........ (kimya kilitawala kwa muda mfupi kidogo huku tukiwa tumekaziana macho). Taratibu nilimsogelea Jenny pale alipokaa, nilimshika mikono yake "twende tukale Jenny na tukimaliza tu kuna zawadi nitakupa" (Jenny alitabasamu baada ya kusikia hivyo)............ SASA ENDELEA

     "Acha kunidanganya Theo, zawadi gani sasa utanipatia?"....
"Aaaaah zawadi ni kitu cha siri, kwahiyo haitokuwa vizuri kuijua kabla ya wakati wake wa kuijua haujafika"....
"sasa mimi si ndiyo mpokea zawadi!, kwahiyo napenda niijue kabla kama ni mbaya niikatae sasa hivi"....
"weeeee, hilo ni bonge la zawadi!, utalipenda mwenyewe tu, ila sikwambii kuwa ni zawadi gani mpaka tukale kwanza tushibe"....
"mmmmnmmmmh, hunikamati kwa huo uongo wako Theo"....
"hiiiiiii, nakwambia ukweli Jenny sikudanganyi, halafu mimi siyo muongo ujue, naongeaga ukweli tu"....
(Jenny alicheka kidogo na kusema) "haya!, kama wewe siyo muongo niambie basi hiyo ni zawadi gani".... 
"kwahiyo wewe unataka kuijua tu hiyo zawadi?"....
"ndiyo"....
"poa, ila itakuwa siyo zawadi tena kwasababu utakuwa tayari unaijua"....
"mimi ninachotaka ni kuijua tu hiyo zawadi, haijarishi kama nitakuwa nimevunja masharti ya zawadi"....
"poa, nakwambia ila kwa sharti moja tu"....
"mmmmmmh!, sharti tena!, sharti gani hilo?"....
"nataka uniahidi, ukiijua tu hiyo zawadi, tunaenda kula"....
"poa, wewe niambie tu"....
(nikawa kimya kwa muda wa dakika moja hivi, nikiwa natafuta neno la kumwambia kisha nilimwinamia karibu na sikio lake la upande wa kushoto) "nitakubeba kukupeleka bafuni wakati utakapoenda kuoga", (nilimnong'oneza).
   Jenny hakukibania kicheko chake cha furaha baada ya kusikia hivyo, alicheka kwa sauti kubwa "halafu Theo wewe"................. ITAENDELEA. 


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.