PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
![]() |
| PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasilino zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya kumi na mbili (12)................ (nilibaki kimya kwa muda kidogo baada ya Jenny kuniambia kuwa hajui chochote kinachoendelea juu ya mabadiliko yake)....
"ila ngoja nikwambie kitu" (Jenny alitaka kuniambia kitu)........................ SASA ENDELEA
"Ehee niambie mke wangu"....
(Jenny alicheka kidogo) "halafu unaonekana kuwa ni muoga ee" (Jenny aliniuliza kwa utani)...
"hapana, mimi siyo muoga aisee ila napenda kujua mapema tu ili tujiandae, maana swala la kuongeza idadi ndani ya familia inahitaji maandalizi makubwa Jenny"....
"sawa, kwahiyo inakuaje sasa?" (Jenny alikubaliana na mimi na kuniuliza)....
"nadhani kwamba kesho nikupeleke kwenye vipimo mke wangu, ili tujue nini kinachoendelea"....
"sawa, mimi nakusikiliza wewe tu"....
"sawa mke wangu".
Siku hiyo nilitamani sana iishe haraka na kuingia siku nyingine kwani nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua sababu ya Jenny kupenda kula vitu vya aina ile.
Asubuhi ya siku hiyo ilipofika, baada ya kumaliza kunywa chai, nilimtaka Jenny ajiandae tayari kuianza safari, nilitoka pale nyumbani kwenda kutafuta usafiri. Nilimkuta Jenny tayari ameshajiandaa, baada ya kurudi pale nyumbani nikiwa na usafiri wa bajaji. Jenny alitoka nje ya nyumba aliposikia mlio wa bajaji, alifunga mlango na kuja kupanda bajaj.
Nilimtaka dereva bajaji atupeleke moja kwa moja hadi Pole Dispensary iliyopo kichangani, ambako palikuwa na rafiki yangu anaefanya kazi hapo. Tukiwa njiani, story za hapa na pale ziliendelea, baina yangu na Jenny lakini zilikuwa haziniingii kabisa kichwani mwangu, kwani nilikuwa naliwazia zaidi tumbo la Jenny.
"je, itakuaje kama kweli Jenny atakuwa na mimba?, na kama ni kweli nitamweleza nini mzee John mpaka anielewe juu ya hili!?" (hayo ndiyo maswali yaliyokuwa yananisumbua sana kwenye ubongo wangu wa ufahamu, lakini sikuweza kuyapatia majibu).
Punde si punde tulifika pale pole dispensary, tulishuka wote na nikamtaka dereva bajaji atusubiri. "Karibuni" (yule rafiki yangu alitukaribisha baada tu ya kuingia mle ndani)....
"asante bwana, mambo vipi"....
"safi tu, za kupotea rafiki yangu"....
"nimepotea wapi ndugu yangu, mimi nipo tu napambana na maisha"....
(yule rafiki yangu alicheka kidogo) "utayaweza lakini?"....
"yatawezekana tu"....
"haya bwana!, karibu shemeji" (yule rafiki yangu alikubaliana na mimi na kumkaribisha Jenny)....
"asante, habari za kazi?"....
"safi tu shemeji, habari za nyumbani"....
"safi tu"....
"sasa, nimemleta huyu shemeji yako, anataka apimwe mimba" (nilimwambia yule daktari ambaye ni rafiki yangu)....
"oooooh, sawa". Yule daktari alimtaka Jenny amfuate, waliingia kwenye chumba kidogo cha kufanyia vipimo.
Baada ya muda mfupi kupita, Jenny alitoka kwenye kile chumba na kuja kukaa pembeni yangu, "vipi huko?" (nilimuuliza Jenny baada tu ya kutoka kwenye kile chumba, nikitaka kujua nini kilichotokea)....
"nimeambiwa nisubiri kidogo, anakuja"....
"poa".
Mara kidogo nilimuona yule daktari akitokea kwenye kile chumba na mkononi akiwa ameshikilia karatasi ya majibu.................. ITAENDELEA

Comments
Post a Comment