PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0654-105503
0692-794942
                              SEHEMU YA 1
     Ilikuwa ni siku ya jumatano naelekea msamvu kituo cha mabasi kwenda kumpokea mgeni ambaye ni mtoto wa shangazi. Kiukweli sikuwa namfahamu kisura japo nilikuwa nalijua jina lake tu, kwasababu mama alikuwa akiniambia story za kumuhusu huyo binamu yangu.
    Nilipofika msamvu kituo cha mabasi sikujua wapi pakuanzia, kwasababu mtu niliemfuata sikuijua sura yake na ukizingatia kwa wakati huo hapakuwa na simu za mkononi. Wakati nikiwa nimesimama huku nimeduwaa, ghafla likaingia basi la Abood pale kituoni likitokea dar es salaam, nililisindikiza kwa macho lile basi mpaka sehemu lilipo simama. Taratibu nilianza kujongea kulifuata lile basi nikidhania niliyefuata labda atakuwa ndani mwa lile basi. Nilipokaribia kufika, moyo ulisita kuendelea kulifuata lile basi na kulazimika nisimame kando kidogo mwa lile basi.
     Macho yangu yakiwa hayataki kabisa kuangalia sehemu nyingine tofauti ya lile basi, abiria wakiwa wanaendelea kushuka. Macho yangu yaliushawishi moyo baada ya kushuka msichana mmoja aliyeumbwa na kaumbika kweli. Kwa njisi alivyo umbika yule msichana nikajikuta nimevutiwa nae, moyoni nilijiambia "daaah sitokubari unipotee machoni pangu, nitakufuata popote uendako". Moyo wangu ukiwa umepigwa butwaa huku macho yangu yakiwa yanamfuatilia vizuri yule msichana ili kufanikisha asiweze kunipotea.
    Ni baada ya kushuka kwenye basi yule msichana na kuchukua mzigo wake ambao ulikuwa ni begi lililokuwa kubwa kiasi. Aliangaza macho huku na kule, kitendo ambacho kilinifanya nigundue kuwa yule msichana alikuwa ni mgeni kabisa ambaye hujawahi kufika mji wa Morogoro, wakati akiwa anaangaza macho yule msichana ghafla macho yetu yakagongana, kitendo ambacho kilimfanya agundue kuwa alikuwa anafuatiliwa. Alichomoa kishikio cha begi lake na kuanza kujongea taratibu akielekea pale niliposimama.
   Mapigo yangu ya moyo yaliongezeka kiasi kwa wasiwasi niliokuwa nao juu ya uzuri wa yule msichana, yalinifanya nishindwe kujua nini cha kumwambia kama akipitia pembeni yangu. "Mambo vipi kaka" ( yule msichana alinisalimia baada ya kufika pale niliposimama)... Poa vipi dada (nikamjibu)... Safi tu, ila samahani kaka... Bila samahani (nilimdakia maneno yake kwa kumtoa wasiwasi)... Naomba kukuuliza kama wewe ni mwenyeji wa hapa morogoro... Ndio, Mimi ni mwenyeji hapa, vipi kwani?... Sawa, mimi nimetoka dar nimeshuka sasaivi hapa, nataka kwenda nane nane lakini sipajui, naomba unielekeze... Sawa ila nane nane ni kubwa sana, sijui unataka kwenda nane nane sehemu gani?... Naenda nane nane maonyesho... Sawa, unaenda kwa nani yako?... Mmmh mbona maswali yamekuwa mengi kaka, kama hutaki kunielekeza basi (yule msichana alichoshwa na maswali yangu)... Kwani wewe si unataka kuelekezwa? (nikamuuliza na kuendelea) nakuuliza hivyo kwasababu na mimi pia nakaa hapo hapo nane nane, sasa ukiniambia unaenda kwa nani naweza kukupeleka mpaka nyumbani kwake na siyo kukuelekeza tu... Asante kaka, naenda kwa mzee mmoja hivi anaitwa John... Huyo mzee John ni nani kwako?... Ni mjomba wangu... Ni mjomba wako!!! (nilistaajabu kusikia hivyo). Nilishindwa kujizuia kuonyesha tabasamu la furaha mbele yake, wakati huo nikiwa nimemduwaza yule msichana kwa kunishangaa, kwanini nimekuwa kwenye hali ile............  ITAENDELEA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.