PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.
![]() |
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasilino zaidi 0692-794942 0654-105503 |
Ilipoishia sehemu ya kwanza (1)....... Nilishindwa kujizuia kuonyesha tabasamu la furaha mbele yake, wakati huo nikiwa nimemduwaza yule msichana kwa kunishangaa, kwanini nimekuwa kwenye hali ile............ SASA ENDELEA....
"Kwahiyo wewe unaitwa Jennifer?"....
"Wewe"!! (yule msichana alistaajabu baada ya kulitaja jina lake, na kuniuliza) wewe umelijuaje jina langu?....
(Nilicheka kidogo kwa furaha, na kumwambia), nijibu kwanza....
"Ndiyo"
Nikiwa mwenye furaha iliyodhihilika mbele ya macho yake na yeye akiwa ameduwaa akishindwa kukiamini kinachoendelea pale. "Dah kweli leo nimeamini kuwa damu ni nzito kuliko maji" nilijikuta najisemea mwenyewe kitendo ambacho kilimfanya yule msichana azidi kuwa na wasiwasi juu yangu. "Kwani wewe ni nani mbona sikuelewi?" (yule msichana aliniuliza), Jenny! mimi naitwa Theo ni mtoto wake wa mzee John, na nipo hapa kwa ajili ya kuja kukupokea, nilikuwa sijui kuwa nitakupataje, ila namshukuru mungu kwa kutukutanisha mapema. Jenny hakusita kuonyesha furaha yake mbele yangu, "siamini ujue, maana nilikuwa sijui kuwa nitawezaje kufika sehemu ambayo sijawahi kufika kabisa, ila mungu ni mkubwa aisee kwa kutufanyanyia wepesi".
"Twende zetu nyumbani basi ukalale maana nahisi umechoshwa sana na safari" (niliongea maneno ya utani niliyoyaambatanisha na kicheko cha furaha)....
"Acha utani Theo" (Jenny aliongea hivyo akiwa anatabasamu)....
"Sasa utani gani Jenny kwahiyo hujachoka?"....
"Mimi sijachoka bwana"....
"Poa, twende zetu basi"....
"Poa", (Jenny alikubaliana na tayari kuanza safari ya kwenda nyumbani), nilimpokea begi lake na kulibeba.
Story za hapa na pale ziliendelea huku tukiwa tunatoka nje ya kituo cha mabasi tayari kutafuta usafiri wa kutufikisha nyumbani. Baada ya kutoka nje ya kituo cha mabasi tulielekea moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha bajaj, ulichukua usafiri na kuanza safari ya kwenda nyumbani. Tukiwa njiani, mziki mzuri uliyokuwa unatuburudisha kwenye ile bajaj ulitufanya tusitamani kufika nyumbani haraka.
"Ama kweli hakuna safari isiyokuwa na mwisho" msemo huu niliuidhirisha pale tu tulipofika nyumbani, hatukuwa na budi kuiacha ile starehe iliyomo kwenye bajaj. Mama alitoka nje ya nyumba baada ya kusikia mlio wa bajaj uliyokuwa ukilia nje ya nyumba yake. Mama alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake pale alipomuona Jenny mbele ya macho yake. "Kaah" Jenny!! (mama alistaajabu baada ya kumuona jenny, alimkimbilia na kumkumbatia).
"Ehee habari za huko utokako mwanangu" (mama alimsalimu Jenny huku wakiwa wanaingia ndani)....
"Safi tu mama sijui nyie hapa"....
"kama ulivyotukuta mwanangu sisi ni wazima wa afya tele"....
"hilo ndio jambo la kumshukuru mungu, aunty"....
"ni kweli mwanangu!,"... (kimya kidogo kilitawala kwa muda mfupi), Theo nenda kachukue juisi.... (nilisimama tayari kwenda kuchukua juisi) . Nilichukua jagi lenye juisi pamoja na grasi, nilimtengea grasi Jenny kisha nikammiminia juisi, nikamimina nyingine kwa ajili yangu.
Tukiwa tunakunywa juisi mimi na Jenny, mama alisimama na kusema "ngoja nikuache mwanangu niandae chakula"...
"sawa aunty" (Jenny alijibu), mama alielekea jikoni tayari kuandaa chakula na kutuacha pale wenyewe tukiwa wawili tu............. ITAENDELEA
Usisahau ku-comment
ReplyDeleteSimulizi ni nzuri sana, hongera sana mtunzi kwa kazi yako nzuri.
ReplyDeleteAsante, endelea kufuatilia kazi zangu
Delete