PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                                               
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA  5

      Ilipoishia sehemu ya nne (4)............... "nitakubeba kukupeleka bafuni wakati utakapoenda kuoga", (nilimnong'oneza).
   Jenny hakukibania kicheko chake cha furaha baada ya kusikia hivyo, alicheka kwa sauti kubwa "halafu Theo wewe"................. SASA ENDELEA. 

    "Nini sasa?" (nikamuuliza Jenny nikiwa nimetabasamu na yeye akiwa bado anacheka)....
"halafu wewe  una utani sana, nani aliyekwambia anataka kubebwa?"....
"Jenny, kwahiyo unataka kuniambia hupendi kubebwa?"....
"ndiyo, kwani mimi mtoto?"....
"hapana, ila wewe ni mwanamke!, na mwanamke ni kama mtoto tu"....
"sasa mimi sitaki"....
"duuuh!, sijawahi kuona mwanamke anaekataa zawadi kubwa Kama hii ila wewe ndiyo wa kwanza"....
"basi mimi ni mwanamke wa kipekee!, heti ee"....
"yani wewe ni zaidi ya kipekee aisee"....
(Jenny alicheka kidogo) "poa bwana, twende".... (Jenny alikubaliana na mimi, alinyanyuka toka kwenye kochi alilokuwa amekaa tayari kwenda kula chakula).
    Tulipofika mezani, nilimsogezea kiti na kumkaribisha akae huku mimi nikiwa nimesimama kando yake mfano wa body guard. "Asante" (Jenny alishukuru baada ya kumfanyia vile) nilisogeza kiti na kukaa kando yake. "Heeeeh!, mlikuwa bado hamjaanza kula tu? " (mama aliuliza kwa mshangao baada ya kufika pale akitokea chumbani kwake).
 "Ndiyo mama" (nilijibu)....
"kwanini sasa Theo, muda wote ule jamani, unamtesa mwenzako na njaa" (mama alinilaumu)....
"hapana aunty siyo kosa la Theo, ila mimi ndiyo nimemwambia siwezi kula bila aunty" (Jenny alinitetea).... 
"kaa! mwanangu mbona unajitesa na njaa lakini"....
"hapana aunty"....
"sawa" (mama aliyakubari maneno ya Jenny).
      Nilichukua maji ya kunawa na kuanza kuwanawisha kisha nikanawa na mimi (tayari kwa kuanza kula). Tukiwa tunaendelea kula story za hapa na pale ziliendelea pia.
    Mnamo majira ya saa mbili za usiku, Baba alirudi kutoka kazini. Jenny alipomuona Baba alisimama na kusalimia "shikamoo uncle", oooh Jenny!, marahaba hujambo (baba aliikubari salamu ya Jenny na kukaa kwenye kochi lake analokaaga). "Sijambo uncle, vipi wewe"....
"Aaaaah!, namshukuru mungu kwa neema yake, maana ndiyo imetufanya tuwe wazima mpaka leo umetukuta tukiwa afya tele kabisa, vipi huko ulikotoka lakini, kwema?"....
"huko, nimekuacha kwema kabisa, mama anakusalimia tu"....
"asante, salamu zake zimefika"....
"sawa uncle"....
"vipi Theo" (baba aliniuliza)....
"safi tu baba, shikamoo"....
"marahaba" (baba aliijibu salamu yangu) "karibu Jenny, hapa umefika kwa mjomba wako, jisikie kama upo dar" (baba alimkaribisha Jenny)....
"asante uncle"....
"sawa" (baba alisimama na kuondoka akielekea chumbani kwake).
     Baada ya siku nne, Mama alitakiwa kwenda kazini, Kwani alikuwa na ruhusa ya siku tatu kwasababu ya kuwa na mgeni ndani ya siku hizo. Jenny alianza kuyazoea mazingira ya pale nyumbani kwahiyo hakukuwa na shida hata akibaki peke yake, kwani na mimi nilikuwa ninashughuri zangu za kuniingizia kipato changu. Kama kawaida ya siku zote mama anapoamka asubuhi ni wajibu wake wa kuandaa chai kisha ndiyo aondoke, lakini kwa siku hiyo haikuwa hivyo kwani chai iliandaliwa na Jenny baada ya kuwamka mapema sana. Mama alifurahishwa sana na Jenny baada ya kufanya vile akiwa anaamini kuwa amepata msaidizi. Baada ya dakika chache kupita, niliwasikia baba na mama wakiwa wanaongea kuhusu mambo yao na ya kikazi pia huku wakiwa wanatoka chumbani kwao. "Za asubuhi Theo" (nilisikia sauti ya baba ikinisalimia)....
"safi, shikamoo"....
"marahaba" (baba aliikubari salamu yangu na kupita)....
"Theo, naacha hela hapa sebuleni mtaenda kuongeza vitafunwa"....
"sawa mama!, shikamoo"....
"marahaba" (mama aliikubari salamu yangu na kupita). Baba na mama niliwasikia tena wakimsalimia Jenny.
    Ni muda mfupi umepita baada ya salamu, kwa muda huo kimya kilitawala. "Jenny, leo naenda kazini mwanangu, kwahiyo tutaonana badae" (nilisikia sauti ya mama ikiwa inamuaga Jenny)....
"sawa aunty, nikutakie kazi njema" (Jenny alijibu na kumtakia kheri)....
"asante mwanangu" (mama alishukuru)....
"Theo, badae" (mama aliniaga)....
"sawa mama (nilijibu).
    Nikiwa bado nipo chumbani kwangu, nikiwa nimejilaza kitandani, ghafula nilisikia mlango wa chumbani kwangu ukigogwa.................. ITAENDELEA.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.