PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                                               
                                                   
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA  6

    Ilipoishia sehemu ya tano (5)........ Nikiwa bado nipo chumbani kwangu, nikiwa nimejilaza kitandani, ghafula nilisikia mlango wa chumbani kwangu ukigogwa..........SASA ENDELEA

     "Theo bado umelala tu? " (Jenny aliniuliza akiwa amesimama nje ya mlango wa chumbani kwangu)....
"hapana Jenny, nimeamka ila nimetulia tu kitandani"....
"poa" (Jenny alikubaliana na mimi kisha akaondoka).
     Hisia kali za kimapenzi juu ya Jenny ziliniandama, huku nikiwa navuta picha yake jinsi alivyo umbika mtoto wa kikaguru. Uzuri wa sura yake, umbo lake, macho yake, dah! kiukweli Jenny aliumbika, alikuwa na kila sifa ya kuitwa mrembo. Kabla, sikuwahi kumuona mwanamke mwingine ambaye ni mrembo zaidi yake. 
     Baada ya kuwaza sana juu ya Jenny bila kupata suruhisho, nikaamka na kuingia bafuni tayari kwa kuoga. Nilirudi chumbani kwangu baada ya kumaliza kuoga, nilichukua pensi na singland kisha nikazivaa, nilitoka mle chumbani na kuelekea subleni. Niliwasha runinga na kuangalia habari na matukio yaliyojili asubuhi hiyo.
    "Mbona leo umechelewa sana kuamka Theo, vipi? (Jenny aliniuliza)....
"aaaaaaah yani leo sijielewi tu kwanini nipo hivi, maana hata kuamka kitandani kwenyewe nimeamka kwa mbinde sana"....
"mmmmh, au unaumwa?".... 
"hapana, siumwi aisee ila nimechoka choka tu"....
"twende tukanywe chai basi upate nguvu" (Jenny alionyesha kunijali juu ya afya yangu)....
"sitaki" (nilimjibu kwa kumkatalia kiutani)....
"kwanini sasa hutaki hata kwenda kunywa chai jamani?" (Jenny aliniuliza kwa sauti lainii na ya unyenyekevu)....
"sijisikii kabisa leo kunywa chai Jenny"....
"mmmmh, basi na mimi sinywi kama wewe hutaki"....
"hapana Jenny, wewe nenda ukanywe, usiniige mimi"....
"yani bora wote tusinywe, maana siwezi kunywa nikiwa peke yangu"....
(nikamwangilia Jenny usoni, nikacheka kidogo).... "sasa unacheka nini?" (Jenny aliniuliza)....
"nakucheka wewe unavyosema hivyo, kwahiyo siku nikiwa sina hamu ya kula na wewe hutokula?"....
"ndiyo"....
(nilimwangalia tena usoni na nikacheka kidogo) "Kumbe ni vizuri kwa kuwa nimepata mwenzangu wa kunisaidia shida zangu"....
(niliposema hivyo, Jenny aliniangalia bila kusema chochote na kukata jicho kulielekeza kwenye runinga).
    Kimya kilitawala kwa muda mfupi, kila mmoja wetu akiwa yupo makini na kuangalia runinga. "Twende basi nikupeleke ukanywe chai Jenny" (niliuvunja ukimya)....
"sitaki unipeleke ila nataka tukanywe wote"....
"poa twende basi" (nilikubaliana na Jenny, nilisogea kwenye runinga na kuizima)... "twende Jenny mbona bado umekaa?" (nilimuuliza Jenny baada ya kumuona bado amekaa)... 
"nakusubiri wewe jamani" (Jenny alinibu na kunyanyuka tayari kwenda kunywa chai)....
     Tukiwa tunaelekea mezani, Jenny alitangulia na mimi nikawa nyuma yake. Mavazi yake aliyoyavaa asubuhi ya siku hiyo yalizidi kunichanganya, kwani yalikuwa yakimuonyesha kwa uzuri kabisa umbile lake jinsi lilivyo. Makalio yake yaliochomoza kidogo kwa nyuma, yalikuwa yanapishana taratibu, "Dah utanitoa roho mwenzako" (nilijisemea moyoni).

     Siku moja nikiwa chumbani kwangu nimejilaza baada ya pilika za hapa na pale nilisikia mlango wa chumba changu ukigogwa, "ingia" (nikaruhusu bila kujua ni nani aliyekuwa anagonga mlango). Nikasikia sauti ya mlango ukiwa unafunguliwa, nilipotupia macho kule niliiona sura ya Jenny..................... ITAENDELEA. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.