PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                                       
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
  SEHEMU YA  7


      Ilipoishia sehemu ya sita (6)........... Siku moja nikiwa chumbani kwangu nimejilaza baada ya pilika za hapa na pale nilisikia mlango wa chumba changu ukigogwa, "ingia" (nikaruhusu bila kujua ni nani aliyekuwa anagonga mlango). Nikasikia sauti ya mlango ukiwa unafunguliwa............ SASA ENDELEA

     Nilipo tupia macho kule mlangoni, niliiona sura ya Jenny inayonichanganya siku zote. Matiti yake yaliyosimama na chuchu zake zikiwa zimechoza pamoja na macho yake yakiwa legevu kama amekula kungu, viliufanya mwili wangu usisimke ghafla. "Asante mungu" (nilijisemea moyoni, nikiwa naamini kuwa mbuzi kafia kwa muuza Supu). Jenny alijisogeza mpaka pale kitandani na kukaa kwenye kitanda "twende tukale" (sauti ya Jenny iliyokuwa nyororo ilisikika)....
"nenda ukale tu, leo sijisikii kula kabisa" (nilimjibu Jenny nikiwa bado nimejilaza kitandani)....
"kwanini?" (Jenny aliniuliza kwa sauti nyenyekevu)....
(kabla sijajibu, nilinyanyuka pale kitandani na kukaa pembeni  yake)....
"Theo, kwanini hujisikii kula?, nijibu basi" (Jenny aliniuliza tena baada ya mimi kuwa kimya na kunisisitiza nijibu)....
"basi tu, sijisikii Jenny"....
"leo nimepika chakula kitamu hicho, twende basi ukale hata kidogo jamani" (Jenny alinibembeleza)....
(nikiwa kimya kidogo nikitafuta neno la kumwambia Jenny) "hata nikienda kula, chakula hakitopanda aisee"....
"weee!, hujakiona chakula cha leo, ukikiona tu wewe ninavyokujua unaweza kula bila kunawa"....
(nikawa kimya huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini)....
"mmmmh, Theo mbona leo sikuelewi kabisa, una matatizo gani kwani?" (Jenny aliniuliza baada ya kuniona kuwa nipo tofauti kabisa na siku nyingine)....
(nilikuwa kimya kidogo nikitafuta neno la kumwambia) "hivi Jenny nitaendelea kuteseka mpaka lini?" (nilimuuliza nikiwa namwangalia usoni)....
"bado sijakuelewa Theo, unatesekaje yani?"....
(nikawa kimya, kwani mdomo wangu ulikuwa mzito kuongea moja kwa moja kile kinachonitesa moyoni)....
"twende tukale basi, hayo mambo mengine tutaongea tukiwa mezani"....
"Jenny, nitawezaje kula na kama sina hamu kabisa ya kula?"....
"mmmmh, kwani Theo nini kinacho kusumbua leo?....
"tatizo ni wewe Jenny"....
(Jenny alishtuka baada ya kusikia hivyo) "mimi tena, nimefanyaje?"....
"Jenny, siku ya kwanza tu kukuona ukiwa unashuka kwenye basi, niliapa kukufuata popote uendako"....
"mmmmh, bado sikuelewi Theo, nini unachokimaanisha"....
(nikawa kimya kidogo) "uzuri wako ulinifanya niduwae pale stendi, nikiwa nakuangalia wewe tu"....
"mmmmmmh" (Jenny aliguna baada ya kusikia hivyo bila kuongea chochote)....
"wewe ndiyo mwanamke pekee uliyeukamata moyo wangu" (niliongea kwa hisia kali)....
"Theo, nini hicho unachokiongea, hujui mimi ni nani kwako?" (Jenny aliniuliza kwa sauti laini, iliyolegea)....
"najua Jenny!, (nilinyamaza kidogo na kuendelea kuongea) najua, wewe ni binamu yangu, kwahiyo sioni kama kuna kosa la kukupenda"....
(Jenny alivuta pumzi kwa kasi na kuiachia kwa kasi pia, na alishindwa kuongea chochote)....
"niambie Jenny, lini mateso yangu yataisha juu yako?"....
(Jenny aliendelea kuwa kimya)....
(nilikuwa kimya pia kwa muda kidogo na kusema) "sasa Jenny ukimya wako unamaana gani?, sifanyi mambo yakawa mazuri kwa sababu yako Jenny, kila ninachokifanya nahisi kukosea kwa sababu yako!, sasa haya yote yataisha lini heti, lini nitakuwa huru juu ya mateso haya Jenny!, (nikawa kimya kidogo na kuendelea) niambie basi niujue mwisho wa mateso yangu Jenny".
    Jenny hakuwa na cha kujibu, alinyanyuka tayari kwa kuondoka huku akiwa amelegea baada ya kutawaliwa na maneno yenye hisia kali. Alipopiga hatua moja tu, niliudaka mkono wake wa kulia kisha nikasimama, nilimvuta Jenny na kuangukia kifuani mwangu................ ITAENDELEA.

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.