PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
![]() |
| PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasilino zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya kumi (10).................... Nilimchukulia Jenny khanga yake na kumpatia "vaa tukaoge" (nilimwambia Jenny baada ya kumpa ile khanga). Jenny aliipokea khanga yake na akaivaa usawa wa matiti kushuka chini, nilimsaidia kunyanyuka kutoka pale kitandani, tulishikana mikono tukiwa tunaelekea bafuni tayari kwa kuoga................. SASA ENDELEA
Tulipomaliza kuoga kila mmoja aliingia chumbani kwake. Nilikuwa mwenye sana siku hiyo kwa kupata kitu ambacho kilikuwa kikininyima furaha siku zote. Nilichukua pensi ambayo nilikuwa naipenda sana kuivaa siku ninayokuwa furaha pamoja na furana yake, na kuzivaa, nilitoka mle chumbani na kuelekea sebuleni. Baada ya muda mfupi, Jenny alitoka chumbani kwake na kuja pale sebuleni. "Twende tukale, mimi njaa inauma" (Jenny alinitaka tukale baada tu ya kufika pale)....
"nilikuwa nakusubiri wewe ujue....
"kumbe!, twende basi....
(nilisimama tayari kuelekea mezani kula chakula alichokiandaa Jenny).
"Vipi, sasahivi chakula kinapanda?" (Jenny aliniuliza akiwa na bonge la tabasamu)....
"aaaah!, yani sasahivi nitakula mpaka unishangae kabisa"....
(Jenny alicheka kidogo, baada ya kusikia hivyo) "haya bwana, na iwe hivyo lakini"....
"usijali Jenny, itakuwa hivyo" (nilinyamaza kidogo na kuendelea kuongea) "nadhani sasahivi mambo yangu yataanza kwenda vizuri kabisa, maana wewe ndiyo ulikuwa unanichanga sana" (niliongea maneno hayo nikiwa namwangalia Jenny usoni, na mkono wangu wa kulia ukiwa umeshikilia kijiko)....
(Jenny alicheka kidogo) "nilikuwa nakuchanganyaje sasa?"....
"nilikuwa nakuwazia wewe tu, jinsi ya kukupa"....
"mmmmh!, kwahiyo ulikuwa hufanyi kazi vizuri kwa sababu yangu?"....
"ndio Jenny".
Jenny alifurahi sana kusikia hivyo, kwani aliugundua upendo wangu juu yake ulivyokuwa umejaa ndani ya moyo wangu, alichota chakula na kunilisha "nakupenda sana Theo" (kile chakula alichonilisha alikisindikaza na hayo maneno)....
"nakupenda zaidi yako Jenny" (nilimjibu, na nikachota chakula na kumlisha). Tukiwa tunaendelea kula, story za hapa na pale zilichangia kuongeza radha ya chakula.
Mapenzi yetu yalizidi kupamba moto kwa kila iitwapo leo, huku tukiwa tunafanya kwa siri sana ili kuepusha wazazi wasiweze kujua..
Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa toka safari yetu ya mapenzi ianze. Siku moja Baba alinitaka niende kazini kwake. Bila hiana muda ulipofika, nilienda kuonana na Baba tayari kukusikia kile alichoniitia.
"Shikamoo baba" (nilitoa salamu kwa baba na kukaa kwenye kuti kilichopo mbele ya meza yake kwa ajili ya wageni waofika pale kikazi)....
"marahaba, vipi shughuli zako zinaendaje?" (Baba aliniuliza kwa kutaka kujua maendeleo ya shughuli zangu"....
"namshukuru mungu, zinaendelea vizuri"....
"basi sawa" (Baba alinyamaza kidogo na kuendelea na kuongea) "sasa nimekuita hapa Theo, kuna kitu nataka nijue kutoka kwako"....
"kitu gani hicho baba" (niliuliza hivyo kwa shauku ya kutaka kukijua ki2 chenyewe)....
(Baba alikuwa kimya kwa dakika chache) "Theo nataka uniambie ukweli, wewe na Jenny, mpoje ukiachana na ubinamu?"....
(nilinyamaza kidogo kwa dakika chache nikiwa napima uzito wa lile swali) "sijakuelewa baba, yani una maana gani ya kuniuliza hivyo?" (nililipinga lile swali la baba na kumuuliza swali)....
"nisikilize kwa makini Theo, wewe na Jenny, mpoje, ukiachana na ubinamu?" (baba aliniuliza tena kwa msisitizo)....
"nikiachana na ubinamu pia Jenny ni rafiki yangu"....
"sawa, ni rafiki yako kivipi?" (baba aliniuliza hivyo kwa kutaka kujua undani wa urafiki wetu)....
"ni rafiki yangu wa kawaida tu Baba"....
(Baba alinyamaza kwa muda kidogo) "naona Theo umeshindwa kujibu vile ninavyotaka, ila jua kuwa mficha maradhi siku zote hua anaumbuliwa na kifo, kwa kuwa umeshindwa kuambia ukweli wa kukuhusu wewe na Jenny, basi sina cha zaidi ila usije ukanihusisha kwa chochote kitakacho tokea kati yenu" (Baba alionekana kama tayari anayajua mahusiano yetu).......................... ITAENDELEA

Comments
Post a Comment