PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                             
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasilino zaidi
0692-794942
0654-105503.
  SEHEMU YA  12

     Ilipoishia sehemu ya kumi na moja (11)................... (Baba alinyamaza kwa muda kidogo) "naona Theo umeshindwa kujibu vile ninavyotaka, ila jua kuwa mficha maradhi siku zote hua anaumbuliwa na kifo, kwa kuwa umeshindwa kuambia ukweli wa kukuhusu wewe na Jenny, basi sina cha zaidi ila usije ukanihusisha kwa chochote kitakacho tokea kati yenu" (Baba alionekana kama tayari anayajua mahusiano yetu)...................... SASA ENDELEA 

     "lakini Baba, hakuna chochote kinachoendelea kati yetu zaidi ya kuheshimiana tu, namuheshimu sana Jenny Baba, namchukulia kama dada yangu wa tumbo moja" (nilizidi kuukwepa mtego wa baba)....
"sawa Theo, ila uelewe msemo huu, pembe la ng'ombe hua halifichiki" (Baba alinyamaza kidogo na kuendelea) "yangu ndiyo hayo tu, kwahiyo unaweza kwenda kuendelea na shughuli zako".... 
"sawa Baba" (nilikubaliana naye, nilibaki kukaa pale kwa muda mfupi nikiwa kimya na wakati huo Baba akiwa anaendelea na shughuli zake). Nilinyanyuka toka kwenye kile kiti na kumuaga Baba tayari kwa kuondoka.
   Nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani baada ya kutoka pale ofisini kwa Baba, niliingia chumbani kwangu baada ya kufika nyumbani na nikajilaza kitandani kuyatafakari yale maneno nilioambiwa na Baba. Niliyatafakari sana yale maneno ila nilishindwa kujua kuwa nitafanya nini kwa wakati ule, "aaah liwalo na liwe" (nilijisemea mwenyewe hayo maneno nikiwa chumbani kwangu nimejilaza kitandani, baada ya kutafakari sana maneno ya Baba na kushindwa kuyapatia ufumbuzi).
    Nilitoka mle chumbani na kuelekea sebuleni, na nikawasha runinga, nikiwa naangalia burudani ya muziki kwenye channel fulani, mara kidogo alikuja Jenny pale sebuleni akitokea chumbani kwake. "Mambo vipi Theo" (Jenny alinipa salamu na kukaa pembeni yangu baada tu ya kufika pale sebuleni)....
"poa vipi Jenny wangu"....
"safi tu, mbona leo umerudi mapema sana, vipi?" (Jenny aliniuliza hivyo, kwani ilikuwa siyo kawaida yangu ya kurudi nyumbani mapema kama siku hiyo)....
"aaaah leo sijisikii vizuri, ndiyo maana nimerudi muda huu, Jenny wangu" (nilimwambia hivyo Jenny kwa nia ya kumdanganya kwani sikutaka ajue chochote kinachoendelea)....
"umemeza dawa tayari?" (Jenny alionyesha kuijali afya yangu, aliniuliza hivyo huku mkono wake wa kushoto akiwa ameushika mkono wangu wa kushoto na mkono wake wa kulia ukiwa upo juu ya kichwa changu akiwa anakitomasa taratibu)...
"ndiyo, nimemeza huko kazini"....
"sawa" (Jenny alikubaliana na mimi na story nyinginezo ziliendelea mahala pale). 
    
     
   Baada ya miezi mitatu kukatika, nilianza kuona mabadiliko ya kimwili kwenye mwili wa Jenny, kwani alianza kupenda kula udongo na kulamba ndimu, kitu ambacho kilikuwa si cha kawaida kwake. Nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya hilo, kwani niliamini kuwa tayari Jenny ana kile kinachomfanya kupenda kula vitu vya aina hiyo.
    Siku moja, majira ya asubuhi tukiwa mezani tunakunywa chai mimi na Jenny, uvumilivu ulinishinda wa kukaa kimya juu ya kile ninachokiona kwa Jenny "mbona siku hizi sikuelewi mke wangu, vipi?"....
"hunielewi kivipi? " (Jenny aliniuliza kabla ya kujibu swali langu)....
"naona siku hizi umebadilika, nipe siri ya mabadiliko yako basi" (nilimuuliza Jenny kiutani utani ila maswali yangu yalikuwa yana maana kubwa sana juu ya Jenny)....
"mabadiliko gani hayo ulioyaona mwilini mwangu, mbona hata mimi mwenyewe sielewi kama nimebadilika"....
"mmmmh mbona siku hizi unapenda sana kula udongo na kulamba ndimu na siyo kawaida yako?"....
(Jenny alicheka kidogo) "mimi napenda tu jamani, kwani ni vibaya?" (Jenny aliniuliza hivyo akiwa anatabasamu)....
"hapana, siyo vibaya ila hizo ni dalili moja wapo za mimba"....
"Jenny alicheka sana kwa furaha baada ya kusikia hivyo) "mimi sielewi bwana"....
(nilibaki kimya kwa muda kidogo baada ya Jenny kuniambia kuwa hajui
chochote kinachoendelea juu ya mabadiliko yake)....
"ila ngoja nikwambie kitu" (Jenny alitaka kuniambia kitu)........................ ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.