PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                         
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA  14

   Ilipoishia sehemu ya kumi tatu (13).............. Mara kidogo nilimuona yule daktari akitokea kwenye kile chumba na mkononi akiwa ameshikilia karatasi ya majibu.................. SASA ENDELEA

   Tulijisogeza pale mezani kwake yule daktari baada ya kufika pale, tayari kwa kuyapokea majibu. "Hongera sana rafiki yangu" (yule daktari alinipongeza kabla ya kuniambia nini kilichotokea)....
"asante sana rafiki yangu" (niliipokea ile pongezi nikiwa natabasamu, ila tabasamu langu lilikuwa ni fake)....
"muda siyo mrefu utaitwa baba, hongera sana kwa hilo rafiki yangu" (yule daktari alizidi kunipongeza) "shemeji ana mimba ya wiki tatu, kwahiyo anahitaji uangalizi wa hali ya juu, mfanye asiwe na mawazo, maana ataweza kuupoteza ujauzito wake, halafu azingatie sana kufanya mazoezi madogo madogo ili kuimalisha afya yake pamoja na afya ya mtoto tumboni" (yule daktari alituambia kilichotokea baada ya vipimo, na kutuelekeza jinsi ya kuilea ile mimba, kisha alimkabizi Jenny ile karatasi ya majibu)....
"asante sana rafiki yangu" (nilitoa shukrani na kumpa mkono kheri).... 
(Jenny alitoa hela kwenye mkoba wake, kiasi cha sh 3000/= na kumpa yule daktari kwa ajili ya malipo ya vipimo)....
"asante sana shemeji" (yule daktari alitoa shukrani yake baada ya kuipokea ile hela).... 
"ngoja tukuache rafiki yangu, sisi tuondoke"....
"sawa, karibuni tena"....
"sawa rafiki yangu" (tulinyanyuka tayari kwa kuondoka).
    Tukiwa njiani tunaelekea nyumbani, Jenny alikuwa mwenye furaha sana siku hiyo, baada ya kujua kuwa ana kiumbe ndani ya tumbo lake, aliitoa ile karatasi ya majibu kwenye mkoba wake na kuisoma vizuri kwa uhakika zaidi. Jenny aliuchukua mkono wangu wa kushoto kwa mkono wake wa kulia na kunishikisha kwenye tumbo lake, "hivi sasa nimekuwa mama kijacho, muda siyo mrefu nitaitwa mama" (Jenny aliongea hayo maneno na kunilalia kwenye bega langu la upande wa kushoto). 
   Furaha ya Jenny haikuishia kwenye ile bajaji tu, tulipofika nyumbani Jenny hakusita kuniambia siri ya mafanikio ya furaha yake "nakupenda sana Theo, leo umenifanya nionekane mwanamke mbele ya wanawake. Sikuwa naamini kama siku moja nitakuwa mama kijacho!, nakupenda sana Theo na nitazidi kukupenda siku zote za maisha yangu, na ninakuahidi kukufuata popote uendako, hata kama ni kaburini sitokuacha peke yako" (Jenny aliyanena hayo maneno kwa hisia kali sana akiwa amenikumbatia, tukiwa sebuleni). "Nakupenda pia Jenny, hakika sitokubari mtu yeyote kulihujumu penzi letu" (niliongea maneno hayo kwa kumuaminisha Jenny lakini moyoni mwangu sikujua nifanye nini!, nilimgandua kifuani mwangu na kumbusu kwenye paji la uso).
    Baada ya hapo, Jenny aliingia jikoni tayari kuandaa chakula cha mchana na mimi nilibaki pale sebuleni, niliwasha runinga na kuangalia burudani ya muziki kwenye channel fulani. "Hayawi hayawi sasa yamekuwa" kweli yamekuwa, sijui nitamweleza nini mzee John?, nitamwanzaje?, na je itakuaje siku akija kujua?", maswali mengi yaliyokosa majibu yalikizonga kichwa changu, yalinifanya nishindwe kustahimili ile hali ya kubaki pale sebuleni. Nilizima runinga na kuingia chumbani kwangu kujilaza kitandani labda huko nikiwa usingizini ndiyo naweza kupata majibu ya maswali yangu.............................. ITAENDELEA 

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.