PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                                     
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
  SEHEMU YA  15

   Ilipoishia sehemu ya kumi na nne (14).................. "Hayawi hayawi sasa yamekuwa" kweli yamekuwa, sijui nitamweleza nini mzee John?, nitamwanzaje?, na je itakuaje siku akija kujua?", maswali mengi yaliyokosa majibu yalikizonga kichwa changu, yalinifanya nishindwe kustahimili ile hali ya kubaki pale sebuleni. Nilizima runinga na kuingia chumbani kwangu kujilaza kitandani labda huko nikiwa usingizini ndiyo naweza kupata majibu ya maswali yangu..................... SASA ENDELEA

     Jenny baada ya kumaliza kupika chakula, alikitenga mezani na kuja kuniita kule chumbani kwangu. "Mbona umejilaza sasahivi mume wangu, vipi?" (Jenny aliniuliza na kukaa kitandani baada ya kuingia mle chumbani kwangu)....
"daaah, najihisi kuchoka tu mke wangu" (nilimjibu Jenny nikiwa bado nimejilaza kitandani)....
"mmmh, mbona leo hujafanya kazi yoyote, umechoshwa na nini mume wangu?" (Jenny alishtuka baada ya kusikia vile)....
"aaaah, basi tu mke wangu, sijielewi aisee"....
(Jenny alianza kupatwa na wasiwasi juu ya ile hali niliokuwa nayo) "au unaumwa mume wangu, niambie basi, mbona unaniacha na maswali yasiyokuwa na majibu lakini"....
"usijali mke wangu, mimi siumwi wala sijisikii chochote kile kibaya unachokihisi, ila nimechoka tu, sijui ndiyo nakusaidia kubeba mimba" (niliongea kwa maneno ya utani ili kumtoa Jenny wasiwasi)....
(Jenny alicheka kidogo kwa furaha, isiyo pimika) "acha utani bwana" (alikikatisha kicheko chake kwa kuongea maneno hayo)....
"siyo utani mke wangu, maana hua nawasikia watu wakiongelea maswala haya, wanasema kuwa  kama mke wako anamimba, halafu muda mwingi unachoka tu wewe mwanamme, basi ujue hapo unamsaidia mkeo kubeba mimba" (nilizidi kuongea maneno yenye utani ili kumtoa Jenny wasiwasi kabisa juu yangu)....
(Jenny alicheka tena kwa furaha kubwa na kukiangushia kichwa chake kifuani mwangu) "acha utani bwana, twende tukale huko" (Jenny alinitaka tukale baada ya kuona utani unazidi)....
(nilinyanyuka na kukaa kitandani, pembeni kidogo na Jenny) "ehee, nimekumbuka!, doktari alisema kuwa ufanye mazoezi madogo madogo, kwahiyo inabidi unibebe hadi mezani"....
"nenda huko, sitaki" (Jenny alikataa kunibeba)....
"mmmmh, kwahiyo hutaki?, ila kwa faida yako ujue!, au njoo nikubebe mimi" (nilimtaka Jenny aje nimbebe baada ya yeye kukataa kunibeba)....
"hapo tena kwenye kubebwa mimi ndiyo napendaga" (Jenny alifurahia baada ya kumtaka aje nimbebe)....
"nenda zako huko, wewe si umekataa kunibeba, na mimi sikubebi" (nilimkatalia Jenny kumbeba na kunyanyuka pale kitandani tayari kuelekea mezani kwa ajili ya kula chakula, nilipopiga hatua kadhaa mbele Jenny alinifuata na kunipanda mgongoni kwa ajili ya kumbeba). Tulielekea mezani Jenny akiwa mgongoni huku akiufurahia utamu wa kubebwa. 
   Mawazo mengi niliyokuwa nayo yalinifanya nianze kukonda siku hadi siku, kitendo ambacho kilimpa Jenny wasiwasi mkubwa sana. Asubuhi ya siku moja tukiwa mezani mimi na Jenny, tukiwa tunakunywa chai "mume wangu mbona siku mwili wako unapungua, una matatizo gani kwani?" (Jenny aliniuliza, akitaka kujua ni nini kinachonisibu na kunisababishia kupungua kwa mwili wangu)....
"mmmmh, mbona nipo sawa mke wangu"....
"sasa, kwanini mwili wako unapungua?"....
"sasa, mwili wangu unapunguaje Jenny, mbona nipo kama zamani tu"....
"hapana Theo, mwili wako umepungua kidogo!, halafu unaonekana kama kuna kitu kinachokusumbua sana wewe, ila hutaki tu kuniambia ukweli, niambie basi na mimi nijue ili nikusaidie kuwazua" ....
(nilibaki kimya kwa muda kidogo) "ngoja nikwambie mke wangu.................. ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.