PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                                         
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
 SEHEMU YA 16

   Ilipoishia sehemu ya kumi na tano (15)................ "hapana Theo, mwili wako umepungua kidogo!, halafu unaonekana kama kuna kitu kinachokusumbua sana wewe, ila hutaki tu kuniambia ukweli, niambie basi na mimi nijue ili nikusaidie kuwazua" ....
(nilibaki kimya kwa muda kidogo) "ngoja nikwambie mke wangu.................. SASA ENDELEA

    "Unajua, wewe unamimba baada ya miezi kadhaa utajifungua na kuanza kulea mtoto, mtoto mchanga atahitaji mahitaji mengi ambayo ni muhimu yatakayo mfanya awe salama muda wote, kwahiyo kinachoniumiza kichwa zaidi ndiyo hicho tu mke wangu" (nilimuongopea Jenny, kwani sikutaka ajue chochote kinachoendelea kwa wakati ule)....
"kwahiyo ndiyo hicho tu mme wangu?"....
"ndio mke wangu"....
"mbona bado mapema sana lakini"....
"ndiyo, ila ni vizuri mke wangu kujiandaa mapema ili hapo badae tusije tukahangaika"....
"basi sawa mme wangu lakini punguza mawazo bwana" (Jenny alikubaliana na mimi na kunisihi nipunguze kuwaza sana)....
"sawa mke wangu, usijali"....
"sawa" (tuliendelea kunywa chai na story za hapa na pale ziliendelea pia). Tulivyo maliza kunywa chai, nilimuaga Jenny na kutoka kuelekea kwenye mihangaiko yangu.
   Sikuwa na furaha kabisa siku hiyo, licha mbele ya Jenny nilionyesha furaha. Kauli ya mzee John alioitoaga kipindi cha nyuma "usije kunihusisha na chochote kitakacho tokea kati yako na Jenny" ilizidi kunichanganya sana na kunisababishia maumivu makali ya kichwa. Maumivu makali ya kichwa yalisababisha nisiweze kufanya kazi yoyote siku hiyo, nilitafuta dawa ya kupunguza maumivu na nikarudi nyumbani. Niliingia chumbani kwangu moja kwa moja na kujilaza kitandani baada ya kufika nyumbani, sikutaka kuonana kabisa na Jenny kwa wakati ule kwani angeniuliza maswali mengi ambayo yalikuwa hayana majibu.

    Ni wiki mbili zimekatika baada ya kuuthibisha ujauzito wa Jenny, ila wazazi walikua bado hawajui nini kinachoendelea kati yetu, (kwani walikuwa wanatoka nyumbani asubuhi sana kwenda kazini na kurudi nyumbani usiku). Usiku wa siku moja nikiwa nimejilaza kitandani, nilikosa kabisa usingizi, "Nitaishi kwa hofu mpaka lini mimi na tumbo la Jenny linazidi kukua tu kila iitwapo leo, itakuaje siku ikija kushtukiwa mimba ya Jenny, kwani nitamuogopa mpaka lini Baba, na kama kutokea tayari imeshatokea?, aaaaaah, liwalo na liwe", (maswali mengi yaliyokuwa yananisumbua kichwani mwangu usiku huo niliyapatia jibu, japokuwa ilikuwa ni ngumu sana kufanya hivyo nilivyotaraji kufanya, ila nilikata shauli kuwa litakalokuwa na liwe, kwani maji ndiyo yameshamwagika tayari na haiwezekani kuyazoa). Kwahiyo sikuwa na sababu tena ya kuuficha ukweli baada ya kugundua kuwa ni lazima hapo badae itakuja kujulikana tu.
   Ilipofika asubuhi ya usiku ule, nilikuwa tayari kuuweka wazi ukweli wa mambo yanayotuhusu mimi na Jenny kwa mzee John. Nilichelewa sana kuamka asubuhi ile kwa sababu nilichelewa sana kulala kwa kuukosa usingizi, ulionisababishia nilale nje ya wakati. Niliingia mezani na kupata breakfast, baada ya kumaliza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kwenye mihangaiko yangu, nilimuaga tayari kwa kuondoka.
   Yalipotimu majira ya saa 7 ya mchana, nilizisitisha shughuli zangu kwa ajili ya kwenda kumuona mzee John. Nilipofika pale kazini kwake, niliingia moja kwa moja ofisini kwake, Baba alishangaa sana kuiona sura yangu mahala pale............................. ITAENDELEA
 
    

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.