PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                                   
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
    SEHEMU YA 17

    Ilipoishia sehemu ya kumi na sita (16)............................. Yalipotimu majira ya saa 7 ya mchana, nilizisitisha shughuli zangu kwa ajili ya kwenda kumuona mzee John. Nilipofika pale kazini kwake, niliingia moja kwa moja ofisini kwake, Baba alishangaa sana kuiona sura yangu mahala pale............................. SASA ENDELEA

   "Shikamoo baba" (nilisalimia na kukaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza yake)....
"marahaba, vipi"....
"safi tu baba, habari za kazi"....
"safi, vipi!, mbona ujio wako ni wa ghafla, kwema huko lakini?" (Baba aliniuliza, kwani alishangazwa na ujio wangu wa ghafla pale kazini kwake)....
"kwema Baba!"....
"ehee, niambie" (Baba alitaka kujua kitu kilicho nipeleka pale)....
(nilikaa kimya kwa muda kidogo, huku nikiwa nimeinamisha kichwa chini nikiwa natafuta neno la kuanza kumwambia Baba)....
"Theo vipi, kuna shida kwani?" (ule ukimya wangu ulimshtua sana Baba)....
"hapana Baba, hakuna shida yoyote"....
"sasa, kwanini upo kwenye hali kama hiyo?"....
(nilikawa kimya tena kwa muda mfupi, Baba alikuwa ananiangalia kwa kushindwa kujua nini kinachonisibu) "Baba, Jenny anamimba!" (niliongea hivyo kwa hofu kubwa, ilionisababishia kuanza kutokwa na kijasho chembamba mwili mzima)....
"nini" (Baba alishtuka sana kusikia hivyo, aliniuliza tena kwa kutaka kujua ukweli zaidi)....
(nilikuwa kimya kwa dakika chache, huku mwili wangu ukiwa umejaa jasho la wasiwasi) "Jenny, ana mimba Baba"....
"unamjua aliyemtia mimba Jenny?....
(nilinyamaza kwa dakika chache) "ndiyo"....
"niambie ni nani na anakaa wapi huyo mtu?" (Baba aliniuliza hivyo kwa shauku kubwa ya kutaka kumjua huyo mtu)....
"ni mimi Baba" (nilijibu hivyo, huku nikiwa natokwa na jasho kila sehemu ya mwili wangu juu hofu kubwa niliyokuwa nayo)....
"nini" (Baba alishtuka sana kusikia hivyo)....
(nilikuwa kimya tu, huku jasho langu la wasiwasi liliendelea kunitoka kiasi cha kuloanisha nguo zilizokuwa mwilini mwangu siku hiyo)....
(Baba alikuwa kimya pia kwa muda kidogo akiwa analipimia uzito lile swala)....
"Theo, hivi dada yako unaweza kumtia kweli?, na umewezaje kufanya hivyo?"....
(sikuwa na majibu ya yale maswali ya Baba, zaidi ya kukaa kimya tu)....
"nijibu Theo" (Baba alinitaka nimjibu baada ya kuniona nipo kimya, lakini sikuweza kufanya hivyo) "sasa umekuja hapa kufanya nini kama hutaki kunijibu?"....
"nimekuja kukupa taarifa Baba ili tujue tunafanyaje juu ya hili" (nilimjibu Baba, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu)....
"kwahiyo sasa hivi ndiyo umeuona umuhimu wangu wa kujua hayo mambo yako, wewe si nilikuita hapa na kukuuliza, lakini ulinikatalia katakata heti oooooh "Jenny ni dada yangu na ninamuheshimu sana kwahiyo siwezi kufanya hivyo!", sasa umewezaje?".... (Baba aliniuliza maswali mengi ambayo yalikosa majibu kwangu) "halafu unakumbuka siku ile nilikwambiaje?!, nilimwambia kuwa "usije kunihusisha na chochote kitakacho tokea kati yako na Jenny", kwahiyo sina cha kukusaidia Theo, utajua mwenyewe cha kufanya"....
"naomba unisamehe Baba" (niliomba msamaha nikiwa nimepiga magoti, machozi yaliyoambatana na kamasi jembamba yalinitoka baada ya kusikia kauli ya mwisho aliyoitoa Baba kuzidi kunichanganya)....
"sina cha kukusaidia Theo, kwanza ondoka hapa, sitaki kusikia kabisa upuuzi wako" (Baba alinitaka niondoke pale kwa kunifukuza)....
    Nilijitahidi sana kuomba msamaha kwa Baba huku nikiwa bado nimepiga magoti lakini haikuwezekana kusamehewa........................ ITAENDELEA



Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.