PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
![]() |
| PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya kumi na saba (17).................... "sina cha kukusaidia Theo, kwanza ondoka hapa, sitaki kusikia kabisa upuuzi wako" (Baba alinitaka niondoke pale kwa kunifukuza)....
Nilijitahidi sana kuomba msamaha kwa Baba huku nikiwa bado nimepiga magoti lakini haikuwezekana kusamehewa........................SASA ENDELEA
Nilitoa kitambaa kwenye mfuko wa suruali yangu na kujifuta machozi pamoja na kamasi, nikiwa bado nimepiga magoti, nilisimama na kuondoka bila kuacha baada ya kumaliza kujifuta machozi pamoja na kamasi. Nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani, niliingia chumbani kwangu na kukaa kitandani baada ya kufika nyumbani.
Sikujua nifanye nini kwa wakati ule kwani akili yangu ilishafika Kiwango cha mwisho kabisa cha kufikiria. Nikiwa bado nimejikalisha pale kitandani, nikiwa sielewi nifanye nini, na kama siri tayari imeshafichuka, ghafla lilinijia wazo la kuondoka kabisa niwe mbali na pale nyumbani. Nilijisogeza taratibu mpaka kwenye droo ya meza yangu ninayohifadhia visent vyangu ninavyopata kwa siku kwenye mihangaiko yangu, iliyopo mle chumbani kwangu. Niliifungua kwa ajili ya kuangalia kiasi cha hela kilichopo ambacho kitaweza kunisaidia mbele ya safari yangu isiyo julikana. Sh 214000 ndiyo kiasi cha hela nilichokikuta kwenye ile droo "aaaaaaah itanitosha sana hiii" (nilijisemea moyoni).
Baada ya kupata jibu sahihi la kuondoka pale nyumbani na kwenda mbali kabisa japokuwa sikujuwa ni wapi, nilimwita Jenny huku nikiwa napanga nguo kwenye begi langu, nilisikia sauti ya Jenny ikiitika kutoka chumbani kwake. Jenny alishtuka sana baada ya kuingia chumbani kwangu na kunikuta napanga nguo kwenye begi langu, "heeee mbona unapakia nguo kwenye begi, una safari ya wapi" (Jenny aliniuliza akiwa amekaa kitandani)....
"nimekuita hapa, nikupe taarifa ya kujiandaa ili tuondoke" (nilimwambia Jenny huku nikiwa naendelea kupakia nguo kwenye begi langu)....
"nijiandae!, ili tuondoke!!, twende wapi Theo?, na kwanini imekuwa ni safari ya ghafla kiasi hiki?" (Jenny aliniuliza maswali mengi, tena kwa mshangao mkubwa, ambayo yalikosa majibu kwangu)....
"Jenny, huu siyo muda wa kuulizana maswali mke wangu, ila nakuomba sana ufanye kile ninachokwambia kwa wakati huu" (nilimkatisha Jenny, kuuliza maswali na kumtaka afanye kile ninachokitaka)....
(Jenny, alianza kububujikwa na machozi kwa kushindwa kuelewa nini kinachoendelea pale)....
"tuondoke!, tunaenda wapi Theo?" (Jenny aliniuliza tena huku akiwa analia lakini sikuweza kumjibu).
Nilipomaliza kupakia nguo zangu kwenye begi langu nilitoka mle chumbani kwangu, nilimuacha Jenny akiwa bado analia, na nikaingia chumbani kwake. Nilichukua begi lililojaa nguo zake na kuliweka kitandani, nililifungua ili kuhakikisha kile kilichomo mle kwenye begi, nililifunga baada ya kuona lilikiwa limejaa nguo zake tu. Nililibeba lile begi na kutoka nalo mle chumbani na kuingia nalo chumbani kwangu.
Nilimkuta Jenny akiwa amekiinamisha kichwa chini, alishindwa kuamini kile alichokiona baada ya mimi kuingia mle chumbani nikiwa na begi lake "Theo, kwanini unanifanyia hivi lakini?" (Jenny aliniuliza akiwa ameduwaa)....
"Jenny mke wangu, naomba unielewe" (niliongea kwa sauti ya chini na ya unyenyekevu mbele ya Jenny)....
"nikuelewe nini?, na hutaki kuniambia!, mimi siwezi kuondoka hapa" (Jenny alionyesha dhahiri kutokubalina na mimi)....
"naomba unisikilize na unielewe vizuri mke wangu"....
"siwezi kukusikiliza wala siwezi kuondoka hapa" (Jenny alichachamaa kutokubaliana na mimi, alichukua begi lake na kurudi nalo chumbani kwake).
Jenny alinicha kwenye mduwazo mkubwa sana baada ya kukataa katakata................ UTAENDELA

Comments
Post a Comment