PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.
![]() |
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya kumi na nane (18)............... "naomba unisikilize na unielewe vizuri mke wangu"....
"siwezi kukusikiliza wala siwezi kuondoka hapa" (Jenny alichachamaa kutokubaliana na mimi, alichukua begi lake na kurudi nalo chumbani kwake)............... SASA ENDELEA
Jenny aliniacha kwenye mduwazo mkubwa sana baada ya kukataa katakata kuondoka pale nyumbani. Akili yangu ilizidi kuchoka, nilijisogeza taratibu mpaka kitandani na kukaa, kisha nikajilaza kichalichali kwa kukikata kitanda nikifikiria cha kufanya baada ya Jenny kukataa kuondoka.
Nilinyanyuka pale kitandani na kumfuata Jenny kule chumbani kwake ili kwenda kumbembeleza mpaka akubari kuondoka, kwani njia iliyobaki ya sisi kuwa salama ni kuwa mbali na pale nyumban. Nilimkuta Jenny akiwa amekaa kitandani na kichwa chake kakiinamisha na mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia tama huku akiwa analia kimya kimya, nilimsogelea taratibu mpaka pale alipokaa, kwa mkono wangu wa kulia nilimfuta machozi yake yaliyokuwa yanadondoka sakafuni.
Nilikaa pembeni yake kidogo pale kitandani nikiwa nimemfyata na mkono wangu wa kulia ukiwa umeushikilia mkono wake wa kulia huku ukiwa unautomasa taratibu ule mkono wa Jenny.
"Nakupenda sana Jenny pia nampenda sana mtoto wangu aliyeko tumboni mwako, nafanya haya yote kwa ajili ya usalama wako pamoja na usalama wa mtoto wetu, inaturadhimu tu kuondoka hapa na kwenda mbali kabisa mke wangu!, kwani unayajua vizuri sana mapenzi yetu jinsi yalivyo mke wangu, ni ya siri sana, sasa wewe una mimba na hio mimba inakua kila iitwapo leo, sasa unajua nini kitatokea kama wazazi wakija kuligundua hili mke wangu?, kwahiyo nakuomba sana mke wangu kubari tuondoke hapa ili tuendako tukawe salama zaidi na mapenzi yetu" (niliongea kwa kirefu sana na kwa sauti ya upole yenye unyenyekevu ndani yake ili kumfanya Jenny aweze kunielewa vizuri, lakini Jenny hakuweza kunijibu chochote kile).
Ukimya wa Jenny ulizidi kunichanganya zaidi, kwani nilishindwa kujua kuwa ukimya wake unamaanisha nini. "Jenny, naomba unijibu mke wangu" (nilimuomba Jenny aweze kunijibu baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kidogo, lakini Jenny hakuweza kunijibu).
Niliumia sana moyoni mwangu baada ya kugundua kuwa Jenny hayupo tayari kufanya kile ninachokitaka. Nilibaki kimya mahala pale huku nikiwa najipa moyo kama Jenny ataweza kubadilisha maamuzi, lakini ukimya wangu haukusaidia chochote.
"Nashindwa kukuelewa Jenny kwa ukimya huo unamaanisha nini?" (nilimuuliza Jenny baada ya kuona kuwa kimya kimezidi)....
(Jenny alibaki kimya kwa dakika chache na kujibu) "Theo, nitawezaje kuondoka na kumuacha aunty ateseke peke yake?, siwezi kuondoka hapa Theo, siwezi....................... ITAENDELEA
Comments
Post a Comment