PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                         
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA 26

   Ilipoishia sehemu ya ishirini na tano (25)..................... "sawa wanangu, lakini huku hakuna nyumba zenye vyumba vya kupangishwa"....
(nilivuta pumzi kwa kasi na kuiachia kwa kasi pia baada ya kusikia hivyo, kwani tulivyokuwa tunaendelea kukaa pale kwenye ile nyumba ya wageni ndiyo hela ilikuwa inatumika sana, na ukizingatia tulikuwa hatuna kazi yoyote ya kutuingizia hela)........................... SASA ENDELEA

  "Lakini pale ninapoishi kuna jilani yangu ana nyumba mbili, na hio nyumba nyingine ni ndogo ni ya chumba kimoja na sebule, sasa subirini badae nikajaribu kuongea naye kesho mtalikuta jibu lenu hapa" (yule mama ntilie alituahidi kuwa anaenda kuongea na jilani yake kuhusu sehemu ya kuishi sisi, mimi na Jenny)....
"sawa mama, tunashukuru sana kwa msaada wako kwetu" (nilimshukuru sana yule mama kwa kunipa ile taarifa ya kwenda kujaribu kuongea na jilani yake)....
"msijali wanangu, mtapata tu" (yule mama ntilie alitupa moyo)....
"asante sana mama" (nilizidi kutoa shukurani zangu kwa yule mama ntilie)....
(kimya kilitawala kwa muda mfupi kidogo, yule mama ntilie akiwa anawahudumia wateja walioingia kwa muda huo)....
"sasa mama, naomba tukuache uendelee na kazi sisi tuondoke, tutaonana badae" (nilimuaga yule mama ntilie, mimi na Jenny tukiwa tumesimama tayari kwa kuondoka)....
"sawa wanangu" (yule mama ntilie alikubaliana na mimi huku akiwa anaendelea na shughuli zake za kuwahudumia wateja wanaoingia pale mgahawani)....
"mama, badae" (Jenny nae aliaga tukiwa tunatoka mle mgahawani).
     Baada ya kutoka pale mgahawani, tulienda moja kwa moja mpaka kwenye ile nyumba ya wageni tulipokuwa tunakaa kwa muda huo.
  "Sasa mme wangu, itakuaje kama hatuna uhakika wa kupata sehemu ya kukaa hapa kijijini?" (Jenny aliniuliza tukiwa tumejilaza kitandani huku akiwa na hofu juu ya kutokuwa na uhakika wa kupata sehemu ya kukaa)....
"usijali mke wangu, Mungu yupo upande wetu, atatusimamia vizuri juu ya hili" (nilimtuliza Jenny kwa kumpa moyo japo na mimi nilikuwa naumiza kichwa juu ya hilo)....
"kwahiyo, hiyo sehemu ambayo ndiyo tunayoitegemea kwa sasa, je itakuaje ikishindikanika mme wangu?, na hapa tunatumia pesa nyingi halafu hatuna kazi yoyote ya kutuingizia pesa, hudhani kuwa tutaaibika mme wangu, sasa tutaishije hapa kijijini?" (Jenny aliniuliza maswali ambayo yalikuwa ni magumu sana kuyajibu, huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya hilo)....
(nilikuwa kimya kwa muda mfupi, nikiyatafakari yale maswali machache ya Jenny lakini yalikuwa ni magumu sana kuyajibu)....
"naomba unisikilize mke wangu, najua fika kuwa tupo kwenye wakati mgumu sana kwa sasahivi, ila nakuomba tupige moyo kwa kipindi hiki kigumu, naamini yatakwisha na tutapata sehemu nyingine ya kukaa hata kama pale pakishindikanika"....
"najua mme wangu lakini kila siku zinavyozidi kwenda mbele ndiyo hali yetu inazidi kuwa ngumu zaidi, na hapa zikipita siku tano tu kama hatujapata sehemu ya kukaa basi hii pesa inayobakia haitotusaidia chochote, sijui tunafanyaje mme wangu?" (Jenny alionekana kuogopeshwa sana juu ya hilo swala)....
(nilikuwa kimya kwa muda mfupi) "naomba tulale mke wangu, kesho tukamsikilize yule mama atakavyosema baada ya hapo ndiyo tujue kuwa tunafanyaje" (nilitaka Jenny tulale kwa nia ya kumkatisha kutoendelea kuuliza maswali kwani yalikuwa yanakiumiza sana kichwa changu)....
"sawa mme wangu" (Jenny alikubaliana na mimi na tulilala huku kichwa chake akiwa amekiweka kifuani mwangu).
    Tukiwa tunakunywa chai, majira ya asubuhi, kwa yule mama ntilie, alikuwa tayari kutupa jibu letu baada ya kuona wateja wamepungia.......................... ITAENDELEA

   
   

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.