PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                                         
                                                         
PENZI  LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
 SEHEMU YA 27

  Ilipoishia sehemu ya ishirini na sita (26)....................... "sawa mme wangu" (Jenny alikubaliana na mimi na tulilala huku kichwa chake akiwa amekiweka kifuani mwangu).
  Tukiwa tunakunywa chai, majira ya asubuhi, kwa yule mama ntilie, alikuwa tayari kutupa jibu letu baada ya kuona wateja wamepungia.......................... SASA ENDELEA

  (Nilijiweka tayari kisaikojia kwa ajili ya kupokea jibu lolote litakalotolewa pale na yule mama ntilie)....
"Nyumba tayari imepatikana wanangu, ila sijaambiwa kuwa ni bei gani atakayowapangishia, kwahiyo nitawaelekeza, kama badae mtakuwa na nafasi mwende pale mkapaone jinsi palivyo, kama mtayaridhia mazingira ya pale basi itakuwa ni vizuri sana maana tutakuwa majilani" (yule mama ntilie alitupa jibu ambalo lilikuwa ni tumaini jipya kwetu)....
"asante nyingi sana kwako mama yetu kwa msaada wako mkubwa sana kwetu", (nilimshukuru sana yule mama ntilie kwa shukurani zangu za dhati)....
"tunaenda sasahivi mama, tukafanye utaratibu hata wa kufanya usafi ili kesho tuhamie" (nilimthibitishia yule mama ntilie kuwa tunaenda muda ule ule akishatuelekeza, kwani tulikuwa na shauku kubwa ya kuiona hio sehemu)....
"sawa!, "Juma, njoo nikutume mwanagu" (yule mama ntilie alimuita Juma, ni mtoto ambae alikuwa anacheza karibu na pale mgahawani) "pale kwa mama yake ashura unapajua?" (yule mama ntilie alimuuliza yule mtoto baada ya kufika pale)....
"ndiyo!, si pale karibu na duka la kina Anifa?" (yule mtoto alikubali na kuhoji ili apate uhakika zaidi hapo anapotumwa)....
"ndiyo pale pale!, sasa wapeleke hawa wageni pale kwa kina Ashura, halafu mkifika pale mwambie hivi mama Ashura, "nimeambiwa niwalete kwako hawa wageni na mama zurufaty", sawa mwanangu" (yule mama ntilie alimuelekeza vizuri sana yule mtoto ili aweze kutufikisha sehemu husika)....
"sawa" (yule mtoto alikubaliana na maelekezo ya yule mama ntilie)....
"asante sana mama, ngoja tufike hapo" (nilitoa shukurani yangu ya mwisho tukiwa tayari kwenda kuiona hiyo nyumba)....
"sawa wanangu" (yule mama ntilie aliipokea shukurani yangu na tukaondoka)
   "Mmmh!, najisikia kichefuchefu mme wangu", (Jenny alinipa taarifa ya kujisikia kutaka kutapika tukiwa njiani tunaelekea huko kwenye hiyo nyumba)....
"aiih, naomba ujizuie mke wangu hadi tufike kwa huyo mama ukapate na msaada pia"....
"hapana mme wangu, siwezi" (Jenny alishindwa kujizuia kutaka kutapika)....
"sasa hapa tupo barabarani mke wangu"....
(Jenny hakujibu chochote, alisogea pendezoni mwa barabara na kuanza kutapika).
   Nilimsaidia kuyafukia yale matapishi baada ya Jenny kumaliza kutapika. "Twende pale basi tukaombe maji ili usukutue" (nilimtaka Jenny twende kwenye nyumba iliyopo jilani na pale barabarani alipotapikia)....
"sawa" (Jenny alikubali huku akiwa anatema mate ambayo yalikuwa yanamghasi mdomoni).
  Tulijisogeza taratibu mpaka hapo kwenye hiyo nyumba, "wenyewe! wenyewwe" nilibisha hodi bila mafanikio ya kujibiwa japokuwa mlango ulikuwa upo wazi. "Nyie kina nani na mnataka nini?, (nilisikia sauti iliyotokea nyuma yetu baada ya kutaka kuondoka mahala pale kwa kujua kuwa tumekosa msaada, niligeuka kwa kutaka kujua ni nani anayetuuliza)....
"shikamoo mzee" (nilisalimia huku tukiwa tunajisogeza taratibu kuelekea pale huyo mzee alipo)....
"marahaba!, vipi, niwasaidie nini?" (yule mzee alituuliza akiwa anatutilia mashaka)....
"samahani mzee wangu, naomba umsaidie mke wangu maji ya kunywa" (nilimuomba yule mzee amsaidie Jenny maji ya kunywa badala ya kusukutua kabla sijamjibu swali lake la kutaka tujitambulishe)....
(yule mzee bila kuhoji, aliingia ndani na baada ya dakika chache kupita alitoka na maji yaliyojaa kwenye kikombe cha plastiki) "asante sana mzee" (nilitoa shukurani yangu kwa yule mzee, niliyapokea yale maji na kumpa Jenny).
  Baada ya Jenny kumaliza kusukutua pia aliyanywa yale maji, nilikichukua kile kikombe toka kwa Jenny alipomaliza kunywa yale maji na kumpatia yule mzee kile kikombe. "Tunashukuru sana mzee wangu" (nilizidi kutoa shukurani zangu kwa yule mzee huku akiwa anakipokea kile kikombe, na kuingia nacho ndani). Ghafla Jenny alianza kulalamika kuumwa na tumbo baada tu ya kunywa yale maji..................... ITAENDELEA






Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.