PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
![]() |
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya ishirini na saba (27).................... Baada ya Jenny kumaliza kusukutua pia aliyanywa yale maji, nilikichukua kile kikombe toka kwa Jenny alipomaliza kunywa yale maji na kumpatia yule mzee kile kikombe. "Tunashukuru sana mzee wangu" (nilizidi kutoa shukurani zangu kwa yule mzee huku akiwa anakipokea kile kikombe, na kuingia nacho ndani). Ghafla Jenny alianza kulalamika kuumwa na tumbo baada tu ya kunywa yale maji..................... SASA ENDELEA
"Babu!, babu" (nilimwita yule mzee akiwa bado yupo ndani mwa ile nyumba ili niweze kumuomba hifadhi ya muda mfupi kwa ajili ya Jenny aweze kuisikilizia hali yake)....
"vipi tena?" (yule mzee aliuliza baada ya kutoka nje na kumuona Jenny akiwa kwenye hali tofauti)....
"mke wangu anasumbuliwa na tumbo, mzee wangu" (nilimwambia yule mzee huku nikiwa namsaidia Jenny kutembea kuelekea kwenye mti uliokuwa umetanda vizuri kwa majani yaliyogandamana akiwa ameinama)....
(yule mzee alirudi tena kuingia ndani na alitoka nje akiwa amebeba mkeka) "mwambie ajilaze humu kwenye mkeka" (yule mzee alinitaka nimwambie Jenny ajilaze kwenye ule mkeka baada ya kumaliza kuutandika pale chini ya ule mti)....
"kwani, imekuaje tena, kijana wangu?" (yule mzee aliniuliza akiwa na wasiwasi juu ya hali ya Jenny)....
"hii ni hali ya kawaida tu kwake mzee wangu wala usiwe na wasiwasi" (nilimwambia hivyo yule mzee kwa kumtoa wasiwasi japo na mimi nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya hali ile iliyojitokeza ghafla kwa Jenny)....
(yule mzee alishtuka sana baada ya kusikia vile) "kwani hua anaumwa mara kwa mara na tumbo?"....
"hapana!, ila pale anapotumia chombo cha plastiki kwa chakula au kunywea maji pamoja na chai, basi hapo ndipo tumbo hua linamsumbua kwa muda mfupi tu na kulejea kwenye hali yake ya kawaida" (niliongea vile kwa kumdanganya yule mzee kwani hata mimi pia sikukijua chanzo cha Jenny kuumwa na tumbo zaidi ya kunywa yale maji)....
"ahaaaah, sasa kwanini usingeniambia tu ili nibadilishe kikombe?"....
"daah!, samahani mzee wangu kwani nilikuwa nahofia kujiona tupo tofauti na wengine, kwasababu ningekwambia hivyo nahisi ungetufikiria tofauti sana mzee wangu....
"sawa!, lakini ungesema tu"....
"nisamehe sana kwa hilo mzee wangu!, sijui tutapata wapi msaada wa usafiri ili nimpeleke hospitalini?" (nilimuuliza yule mzee kama kutakuwa na uwezekano wa kupata usafiri ili niweze kumpeleka Jenny kwenye matibabu)....
"haina haja ya kwenda huko hospitalini kijana wangu!, (yule mzee aliikataa ile habari ya kumpeleka Jenny hospitalini) "kwani hilo tumbo linakuumaje Bibi?" (yule mzee alimuuliza Jenny kwa kutaka kujua ili aweze kufanye kitu fulani)....
"linasokota hapa chini ya kitovu" (Jenny aliongea kwa shida sana kwasababu ya yale maumivu ya tumbo aliyokuwa anayasikia)....
"oooooh!, basi kuanzia leo umepona Bibi, hilo tumbo halitokusumbua tena, sawa ee!, (yule mzee baada ya kusikia vile, aligundua kitu fulani kinachomsumbua Jenny tumboni mwake, aliinuka na kuingia ndani mwa ile nyumba)....
"mmmh, tumbo linauma sana mme wangu"....
"usijali mke wangu utapona tu, kwani nahisi huyu mzee ni mtaalam wa miti shamba" (nilimfariji Jenny na kumpa moyo)....
(kimya kilitawala kwa muda mfupi huku Jenny akiwa anayasikilizia maumivu ya tumbo lake, mara kidogo yule mzee alikuja pale tulipo akitokea ndani mwa ile nyumba akiwa amebeba kikombe kile kile cha plastiki kilichokuwa na maji ndani yake)....
"hii siyo sumu, ila ni dawa kiboko ya tumbo, hata kama tumbo lako likiwa linauma vipi ila ukitumia hii dawa maumivu yanaisha papo hapo na hutaumwa tena na tumbo" (yule mzee aliipamba ile dawa kwa maneno matamu ya kuisifia, alijimiminia kidogo ile dawa kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto na kuilamba, alifanya hivyo kwa ajili ya kuihakikisha kuwa ile dawa ilikuwa ni salama, kisha alimpatia Jenny ile dawa baada ya yeye kuionja, Jenny aliipokea ile dawa na kuinywa yote).
Baada ya muda mfupi kupita, jenny alianza kulia juu ya maumivu makali sana ya tumbo aliyokuwa anayasikia baada ya kunywa ile dawa....................... ITAENDELEA

Comments
Post a Comment