PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                                 
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
  SEHEMU YA 29

    Ilipoishia sehemu ya ishirini na nane (28).................... "hii siyo sumu, ila ni dawa kiboko ya tumbo, hata kama tumbo lako likiwa linauma vipi ila ukitumia hii dawa maumivu yanaisha papo hapo na hutaumwa tena na tumbo" (yule mzee aliipamba ile dawa kwa maneno matamu ya kuisifia, alijimiminia kidogo ile dawa kwenye kiganja cha mkono wake wa kushoto na kuilamba, alifanya hivyo kwa ajili ya kuihakikisha kuwa ile dawa ilikuwa ni salama, kisha alimpatia Jenny ile dawa baada ya yeye kuionja, Jenny aliipokea ile dawa na kuinywa yote).
   Baada ya muda mfupi kupita, jenny alianza kulia juu ya maumivu makali sana ya tumbo aliyokuwa anayasikia baada ya kunywa ile dawa....................... SASA ENDELEA

   "Mbona hali yake imezidi kuwa mbaya, vipi mzee wangu?" (nilimuuliza yule mzee huku nikiwa mwenye wasiwasi mkubwa sana juu ya hali ya Jenny kuzidi kuwa mbaya baada ya kunywa ile dawa)....
"usijali kijana wangu, hapo dawa ndivyo inavyofanya kazi, muda mfupi tu atakuwa yupo katika hali yake ya kawaida kabisa na hatosumbuliwa tena na tumbo" (yule mzee alinitia moyo na kunipa maelekezo juu ya dawa inavyofanya kazi)....
"hapana mzee wangu siwezi kuivumilia hii hali, unamuona mtu anavyolia juu ya maumivu makali anayoyasikia halafu unaniambia nisiwe na wasiwasi, wewe mzee vipi, au unataka kuniulia mke wangu?" (nilishindwa kukubaliana naye yule mzee na kumshutumu kwa maneno makali kwani hali ya Jenny ilizidi kuwa mbaya mara dufu)....
"najua kuwa unaumia sana juu ya hali ya mwenzako kuwa mbaya, lakini hii hali ni ya muda mfupi tu na atarejea kwenye hali yake ya kawaida kabisa, kwahiyo kuwa mvumilivu kidogo tu kijana wangu" (yule mzee alizidi kunitia moyo kwa maneno ya faraja)....
"Theo, nakufa miye!, nakufa mme wangu" (Jenny alionekana kukata tamaa kabisa ya kuishi juu maumivu makali aliyokuwa anayasikia tumboni mwake)....
"huwezi kufa mke wangu, huwezi, utakuwa salama muda mfupi tu" (nilimtia moyo Jenny huku nikiwa natokwa na machozi ya uchungu mkubwa niliokuwa nao juu ya hali yake kutoniridhisha)....
"nakufa mie, nakufaa!, mama nakufa huku mwanao, naomba unisamehe mimi" (Jenny alizidi kuongea maneno ya kukata tamaa ya kuendelea kuishi)....
"usiongee hivyo mke wangu, huwezi kufa wewe, utakufaje sasa na kuniacha peke yangu, hapana mke wangu, hapana, huwezi kufa" (niliongea maneno ya kukata tamaa juu ya hali ya Jenny, huku nikiwa naendelea kutokwa na machozi)....
   Nilimkunja tai yule mzee kwa machungu makubwa niliyokuwa nayo "umempa nini mke wewe mzee?" (nilimuuliza yule mzee nikiwa bado nimemkunja tai) " sasa sikiliza, mke wangu akifa tu na wewe pia ni lazima ufe, nakuua!" (nilimtishia maisha yule mzee nikiwa bado nimemkunja tai na sura yangu ya kawaida ilibadilika kabisa na kuwa kama sura ya gaidi).
   "Naomba nikuache kidogo mke wangu nikatafute usafi wa kwenda hospitalini" (nilimbusu Jenny kwenye paji la uso, baada ya kumwambia hivyo kisha nikasimama na kuondoka tayari kwenda kutafuta usafiri).
  Sikujuwa ni wapi pa kuanzia kutokana na ugeni niliokuwa nao pale kijijini, nilizunguka huku na kule kutafuta usafiri lakini haikuwa rahisi kupata. Nilikata tamaa kabisa ya kupata usafiri, niliamua kurudi kwa Jenny ili nikajue njia nyingine ya kuweza kumsaidia Jenny na kuwa salama. Nikiwa njiani narudi kwa Jenny huku nikiwa sijitambui kabisa kwa jinsi nilivyojawa na mawazo juu ya hali ya Jenny, ghafla nililiona gari dogo likiwa linakuja, nikalisimamisha kwa ishara ya kupungia mkono, yule dereva wa lile gari alipunguza mwendo na kusimama kandoni mwa barabara. "Habari yako ndugu" (nilimsalimia yule dereva, aliyekuwa ni kijana wa lika kama langu)....
"safi, nikusaidie nini?" (yule kijana aliniuliza baada tu ya kupokea salamu yangu)....
"samahani sana ndugu yangu, japo sijui kuwa unaenda wapi ila nakuomba sana msaada wa usafiri wako ukamsaidie mke wangu kumpeleka hospitalini kwani anaumwa sana" (niliongea maneno ya kutia huruma ili niweze kukubaliwa ombi langu)....
"daah!, yuko wapi?"....
"yuko hapo tu mtaa wa nyuma ndugu yangu"....
(yule kijana alikuwa kimya kwa dakika chache) "sawa!, panda hapo twende" (yule kijana alilikubali ombi langu na kuniamuru nipande kwenye gari tayari kwenda kumsaidia Jenny kumpeleka hospitalini).
  Baada ya kufika pale kwa yule mzee nilipomuacha Jenny nikiwa na usafiri, nilishtuka sana baada ya kumuona Jenny akiwa tayari...................... ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.