PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.

                                                       
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA 30

  Ilipoishia sehemu ya ishirini na tisa (29)...................... "yuko hapo tu mtaa wa nyuma ndugu yangu"....
(yule kijana alikuwa kimya kwa dakika chache) "sawa!, panda hapo twende" (yule kijana alilikubali ombi langu na kuniamuru nipande kwenye gari tayari kwenda kumsaidia Jenny kumpeleka hospitalini).
  Baada ya kufika pale kwa yule mzee nilipomuacha Jenny nikiwa na usafiri, nilishtuka sana baada ya kumuona Jenny akiwa tayari...................... SASA ENDELEA

  Amepona. Kwa hali ile mbaya niliyomuacha nayo Jenny sikuweza kuamini kama nitamkuta katika hali yake ya kawaida, nilimkimbilia na kupiga goti mbele yake "mke wangu, umepona?" (nilimuuliza Jenny kwa mshangao mkubwa huku nikiwa nampapasa papasa kwenye mashavu)....
"ndiyo mme wangu, niko na afya njema sasahivi"....
(nilimkumbatia Jenny baada ya kusikia vile) "ulikuwa na hali mbaya sana mke wangu, nilienda kutafuta usafiri ili nikupeleke hospitalini" (nilimwambia hivyo Jenny nikiwa bado nimemkumbatia huku chozi la furaha likinidondoka)....
"usijali mme wangu, nashukuru mungu nipo salama kabisa"....
"asante sana ndugu yangu kwa kujitolea kunisaidia, pia naomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, maana kwa hali niliyomuacha nayo mke wangu ilikuwa mbaya sana ila namshukuru mungu kwa kumrejeshea afya yake" (nilitoa shukurani zangu za dhati kwa yule dereva wa ile gari ndogo baada ya kumwachia Jenny, pia nilimuomba radhi kwa kile kilichojitokeza kwani sikutegemea kama nitaweza kumkuta Jenny akiwa kwenye hali yake ile niliyomkuta nayo)....
"hamna shida ndugu yangu, ni jambo la kumshukuru mungu kama mke wako yuko salama" (yule dereva aliipokea radhi yangu, aliwaaga Jenny pamoja na yule mzee kisha akaondoka)....
(nilipiga magoti mbele ya yule mzee tayari kumuomba msamaha juu ya yale yaliojitokeza) "naomba unisamehe mzee wangu"....
"usipige magoti kijana wangu, kaa hapo na mwenzako" (yule mzee aliyakataa magoti yangu na kunitaka nikae karibu na Jenny)....
"naomba unisamehe sana mzee wangu" (niliusisitizia msamaha wangu kwa sauti ya upole kwa yule mzee nikiwa bado nimepiga magoti)....
"sawa, lakini na mimi ninakuomba inuka ukae hapo na mwenzako" (yule mzee aliyakataa kabisa magoti yangu, niliinuka na kukaa karibu na Jenny kama vile anavyotaka)....
(kimya kilichukua nafasi yake kwa muda mfupi kidogo huku nikiwa namsikilizia yule mzee kuwa atasema nini juu ya kile kilichotokea) "kijana unaitwa nani?" (yule mzee aliniuliza baada ya kimya cha muda mfupi kupita)....
"naitwa Ally Abdala"....
"mmetoka wapi?"....
"tumetoka Dodoma"....
"mpo hapa kijijini kwa ajili ya shughuli gani?"....
"hatuna shughuli maalum iliyotuleta hapa, ila tumekuja kutafuta maisha kwahiyo kwa shughuli yoyote itakayojitokeza mbele yetu tunafanya"....
"sawa" kwahiyo mna muda gani hapa kijijini kuanzia mfike?"....
"hadi leo tuna siku ya tano mzee wangu"....
"sawa, karibuni sana hapa kijijini kwetu vijana wangu"....
"asante sana mzee wangu"....
"kijana wangu, yafute akilini mwako yale mambo yaliyotokea, kwani sasa yameshapita tayari, najua kuwa siyo akili yako iliyokuwa inakutuma kusema vile ila zilikuwa ni hasira tu baada ya kumuona mwenzako yupo katika hali mbaya ambayo ilikufanya ushindwe kuivumilia, nimependezwa sana na tabia yako, unapokosea unajua kuwa umekosea na unajishusha, pia una upendo wa dhati kwa mke wako nimependezwa sana na hili, nimegundua kuwa nyie ni mwili mmoja kweli, mmoja akiumua yale maumivu mnayasikia wote, mnapendeza sana, "asante sana mzee wangu" (nilidakia kwa kutoa shukurani zangu za kusifiwa juu ya mwenendo wa mapenzi yetu, kisha yule mzee aliendelea kuongea), mimi naitwa mzee Jakob hivi mnavyoniona ndivyo nilivyo, mke wangu alikufa miaka miwili iliyopita na kwa bahati mbaya hatukuweza kupata mtoto, "pole sana mzee wangu" (nilimdakia tena yule mzee kwa kumpa pole baada ya kusikia kuwa amempoteza mke wake, na aliendelea kuongea), asante sana kijana wangu, pia nataka niwaambie kitu kimoja ambacho kitakuwa ni cha muhimu sana kwenu......................... ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.