PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                                 
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   SEHEMU YA 20

   Ilipoishia sehemu ya kumi na tisa (19)...............  "Nashindwa kukuelewa Jenny kwa ukimya huo unamaanisha nini?" (nilimuuliza Jenny baada ya kuona kuwa kimya kimezidi)....
(Jenny alibaki kimya kwa dakika chache na kujibu) "Theo, nitawezaje kuondoka na kumuacha aunty ateseke peke yake?, siwezi kuondoka hapa Theo, siwezi................. SASA ENDELEA

    Nilishtuka sana baada ya kusikia hilo jibu alilolitoa Jenny, nilivuta pumzi kwa kasi na kuiachia kwa kasi pia, na nikabaki kimya kwa dakika chache nikiwa napima uzito wa lile jibu la Jenny huku nikitafuta maneno mengine ya kumwambia ambayo yatakuwa mazito kulishinda jibu lake. "Jenny, unataka hadi mimi nife ndiyo ujue kuwa naumia kiasi gani juu ya hili?,....
"kwanini unasema hivyo mme wangu lakini?" (Jenny aliniuliza hivyo akiwa na hofu juu ya swali langu nililomuuliza).....
"nijibu kwanza, unataka hadi mimi nife ndiyo ujue kuwa nina maumivu kiasi gani ndani ya moyo wangu?" (nilimtaka Jenny anijibu, baada ya kuniuliza swali lake bila kujibu swali langu)....
"hapana mume wangu, sitaki kukupoteza"....
(nilikuwa kimya kwa dakika chache baada ya kusikia hilo jibu la Jenny)  "sawa!, kama kweli hutaki kunipoteza basi fanya kile ninachokwambia Jenny, (niliongea hivyo na kusimama), naenda kutafuta usafiri, nije kukuta tayari umeshajiandaa" (baada ya kumaliza kuongea hayo, nilitoka nje tayari kwenda kutafuta usafiri wa kutufikisha stendi).
   Nilimuacha Jenny pale chumbani kwake, kwenye wimbi zito la mawazo kwani hadi hapo hakujua nini kinachotusababishia sisi kuondoka pale nyumbani kwa haraka vile. Nilirudi nyumbani baada ya kupata usafiri wa bajaji, nilimtaka dereva bajaji asubiri kisha nikaingia ndani. Nilienda moja kwa moja hadi chumbani kwa Jenny, nilimkuta Jenny analia lakini alikuwa tayari amejiandaa kwa safari.
   Nilisogea mpaka pale alipokaa, nikapiga magoti mbele yake na kwa mikono yangu nilimfuta machozi yake "siyo muda wa kulia huu mke wangu, usafiri upo hapo nje unatusubiri" (niliongea hivyo huku nikiwa namfuta machozi yake taratiiiiibu). Nilichukua begi lake la nguo na kutoka nalo nje tayari kwenda kulipakia kwenye ile bajaji iliyokuwa inatusubiri pale nje, niliingia chumbani kwangu na kuchukua begi langu la nguo tayari kwenda kulipakia nalo pia. Nilirudi chumbani kwa Jenny baada ya kuona kuwa Jenny hatoki mle chumbani kwake, "twende mke wangu, kila kitu kitakuwa sawa huko tuendako" (niliongea hivyo huku nikiwa nimemshika mikono yake tayari kumsaidia kunyanyuka)....
"kwani tunaenda wapi lakini?" (Jenny aliniuliza swali ambalo lilikuwa ni gumu sana kwangu kwani hata mimi sikujua ni wapi tunapotaka kwenda)....
"usijali mke wangu, utajua tu tukishafika stendi" (nilimjibu Jenny huku nikiwa nachukua mkoba wake). Jenny hakuwa na lingine zaidi ya kunisikiliza tu, taratibu tulijikokota tukiwa tumeshikana mikono tukielekea nje tayari kuianza safari.
   Tukiwa njiani tunaelekea stendi ya mabasi, tulikuwa tunaburudishwa na mzuki mzuri uliyopo kwenye ile bajaji lakini kila mmoja alikuwa yupo busy kwa kuiwazia hiyo safari isiyojulikana. Tulishuka kwenye ile bajaji baada ya kufika pale stendi, nilishusha mabegi yetu na kumpatia hela yake yule dereva bajaji. Tuliingia ndani ya stendi huku nikiwa nimebeba mabegi yote mawi.
  Tukiwa ndani ya stendi, niliduwaa baada ya kuona wingi wa mabasi yaliyopo pale stendi na sikujua wapi pa kuelekea........................... ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.