PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.
![]() |
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya thelathini (30)................... mimi naitwa mzee Jakob hivi mnavyoniona ndivyo nilivyo, mke wangu alikufa miaka miwili iliyopita na kwa bahati mbaya hatukuweza kupata mtoto, "pole sana mzee wangu" (nilimdakia tena yule mzee kwa kumpa pole baada ya kusikia kuwa amempoteza mke wake, na aliendelea kuongea), asante sana kijana wangu, pia nataka niwaambie kitu kimoja ambacho kitakuwa ni cha muhimu sana kwenu......................... SASA ENDELEA
"Eheee, tuambie mzee wangu" (nilimuhimiza yule mzee atuambie hicho kitu kwani nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kukijua kuwa ni kitu gani)....
(yule mzee alinyamaza kwa dakika chache) "kabla sijawaambia kwanza ningependa kujua kuwa kwa sasa mnakaa wapi, sehemu mliyofikia?"....
"tumefikia kwenye nyumba ya wageni iliyopo pale karibu na stendi, ila kwa sasa tunatafuta nyumba ya kupanga kwani pale tulipo kwenye ile nyumba ya wageni tunatumia gharama kubwa sana halafu hatuna kazi yoyote inayotuingizia kipato, sasa tulikuwa tunaelekea kwa mama mmoja hapo mtaa wa mbele, tumeelekezwa hapo, kufika pale vile mwenzangu akaanza kusumbiliwa na kichefuchefu na kuanza kutapika, tukaona bora tuje hapa ili tuombe msaada wa maji, ndiyo tupo hapa mpaka sasahivi" (nilimweleza vizuri sana yule mzee japo maneno mengine nilimdanganya kwasababu ya kuusalimisha usalama wetu katika kile kijiji)....
(yule mzee alinyamaza kwa muda mfupi baada ya kumaliza kutoa maelezo yaliyojitosheleza kwa swali lake) "hiyo yote ilikuwa ni mipango ya mungu ya nyie kufika mahala hapa"....
"kwanini unasema hivyo?" (nilimuuliza yule mzee baada ya kusema kufika kwetu kwa yule mzee ilikuwa ni mipango ya mungu)....
(yule mzee alinyamaza kwa dakika chache) "ni miaka miwili sasa imepita toka mke kipenzi afariki, kwahiyo toka wakati huo mke wangu alipofariki mimi nikabaki mpweke mahala hapa mpaka leo hii kwani aliyekuwa furaha yangu ni mke wangu pekee, nilitengwa na ndugu zangu wote kwasababu ya mwanamke niliyekuwa nampenda sana lakini wao hawakumpenda, hiyo ndiyo sababu kubwa pia ya mimi kuishi peke yangu, hizo nyumba mbili mnazoziona ni nyumba zangu nilizojenga pamoja na mke wangu, hiyo nyumba kubwa nakaa mimi na hiyo nyumba ndogo haina mtu wa kukaa, (alinyamaza na kuendelea) hivi mnajua ni kwanini nimeweza kuwaambia haya yote?" (yule mzee alituelezea mambo mengi yaliyomsibu na mwishowe alituuliza kama tumeweza kujua kuwa ni kwanini ameamua kutueleza yale mambo yote)....
"hapana mzee wangu, ila pole sana kwa mambo yote yaliyokukuta" (nilimpata pole yule mzee baada ya kujua kuwa amekumbwa na mambo mazito sana)....
"asante sana kijana wangu, sababu kubwa iliyonifanya niweze kuwaambia haya mambo yote ni kwamba nimechoka kuwa mpweke, nahitaji furaha ila hiyo furaha inatoka kwenu kama mtaweza kunikubalia ombi langu"....
"ombi gani hilo?"....
"ombi lenyewe ni dogo tu lakini lina umuhimu mkubwa sana kwangu, ni kwamba napenda sana tuishi hapa pamoja, nitawapa hiyo nyumba ndogo mtakuwa mnakaa humo
bure kabisa bila gharama yoyote ile, na msimu wa kilimo ukifika nitawapa shamba la kulima vijana wangu" (yule mzee alituomba tuweze kuishi nae pale kwa kutufanya kuwa kama wanawe)....
"tunashukuru sana mzee wangu kwa kutufanya kuwa kama wanao, hilo swala halina mjadala kwetu limepita moja kwa moja" (nilimshukuru sana yule mzee kwa kutupatia nyumba ya kuishi bila gharama yoyote, nilifurahi sana siku hiyo)....
"sawa, na mimi nawashukuru pia kulikubari ombi langu" (yule mzee alitushukuru pia, kile kitendo cha kutushukuru kilinifanya nigundue kuwa alikuwa ni mzee mwenye busara sana).
Safari ya kwenda kwa yule mama tulioelekezwa na yule mama ntilie iliishia pale pale kwa yule mzee. Yule mzee alianza kututembeza katika eneo lake lililozunguka nyumba zake huku stori za hapa na pale zikiwa zinaendelea. "Sasa babu, tunaomba tukuache mara moja tu ili tukachukue kilichochetu pale kwenye nyumba ya wageni"....
"sawa vijana wangu" (yule mzee alikubaliana na mimi, tuliondoka na kumuacha mzee Jakob akiwa mwenye furaha sana, tulielekea moja kwa moja kule kwenye nyumba ya wageni tayari kwenda kuchukua kilichochetu ili kuhamishia makazi mapya kwa yule mzee).
Niliogopa sana baada ya kukalibia kufika kwenye ile nyumba ya wageni na kuwaona askari polisi waliokuwa wamebeba bunduki wakiwa wamejaa kwa kuizunguka ile nyumba ya wageni......................
Unajua nini kilichofuata?,
Basi usikose sehemu ifuatayo..
Comments
Post a Comment