PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                             
                                                                 SEHEMU YA 21
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
   

    Ilipoishia sehemu ya ishirini (20)................ Tulishuka kwenye ile bajaji baada ya kufika pale stendi, nilishusha mabegi yetu na kumpatia hela yake yule dereva bajaji. Tuliingia ndani ya stendi huku nikiwa nimebeba mabegi yote mawili.
  Tukiwa ndani ya stendi, niliduwaa baada ya kuona wingi wa mabasi yaliyopo pale stendi na sikujua wapi pa kuelekea...................... SASA ENDELEA

  Niliangaza macho huku na kule ili kuona kama kutakua na basi lolote ambalo lilikuwa tayari kwa kuianza safari kwa muda ule, ghafla niliiona basi la kamwana, linalofanya safari zake za kiteto morogoro likiwa tayari kwa kuondoka. "Twende mke wangu tukapande lile basi nadhani halina muda mrefu linaondoka" (nilimwambia Jenny), Jenny hakuwa na neno, alinifuata nyuma yangu. Nilimuomba kondakta wa lile basi atuhifadhie mabegi yetu kwenye buti na yule konda alifanya hivyo, na sisi bila kuchelewa tuliingia kwenye basi tayari kusubiri muda wa kuanza safari ufike.
  "Njaa inauma mme wangu" (Jenny alilalamika kuumwa na njaa, kwani baada ya kumaliza kunywa chai majira ya asubuhi Jenny hakupata tena nafasi ya kupika chakula cha mchana kwa sababu ya misukosuko ya hapa na pale juu ya ile safari na hatukuweza kula chakula chochote cha mchana)....
"naomba unisubiri basi nikatafute chakula hapo nje"....
"sawa". (Jenny alikubaliana na mimi, nilitoka nje mwa lile basi na kumuacha Jenny tayari kwenda kutafuta chakula). 
   Nilimfuata kondakta wa lile basi kwa ajili ya kumtaarifu ili wasije kuniacha kwenye mataa, "fanya haraka, kwani hatuna muda mrefu tunaondoka" (yule kondakta alinitaka nisichelewe huko niendako).
  Nilienda moja kwa moja mpaka kwenye kitanda panapokaangwa chipsi, na kununua sahani mbili za chipsi, samaki wawili wa kuchomwa, juisi mbili pamoja na maji makubwa mawili na kurudi kwenye basi. "Asante" (Jenny alitoa shukrani yake baada ya kumpatia sahani moja ya chipsi iliyofungwa kwenye mfuko wa lambo laini)....
"poa mke wangu" (niliipokea shukrani yake na kwa pamoja tulianza kula). 
   Ni dakika chache tu baada ya kuanza kula, nilisikia sauti ya spika iliyofungwa kwenye lile basi ki-automatically ikitutaarifu kuwa basi lipo tayari kuianza safari, kwahiyo tujiandae kwa safari. Moyo wangu ulijawa na furaha baada ya kiivyo, kwani nilikuwa bado nina hofu tulipokuwa bado tunakawia kuondoka pale stendi. 
   Tulipokuwa njiani baada ya kuianza safari, tulikuwa tunaburudishwa kwa kuangalia season nzuri kabisa ya "legend of the seaker" lakini haikuwa rahisi kwangu kuifurahia ile season kwani mawazo ya kwenda kuyaanza maisha mapya katika makazi mapya yalikuwa yananizonga.
   Mnamo majira ya saa mbili za usiku, basi lilingia kwenye kituo kidogo cha mabasi katika kijiji cha matui kilichopo wilaya ya kiteto. Nilimwamsha Jenny, aliyekuwa amelala kwa kukiegemeshea kichwa chake kwenye bega langu la upande wa kushoto tayari kwa kushuka mahala pale.
  Baada ya kushuka pale stendi, nilifuata konda na kumtaka atutolee mabegi yetu toka kwenye ile buti alimoyahifadhi. Nikiwa nimesimama kandoni mwa lile basi huku nimeshikila mabegi na Jenny akiwa ameniegemea kwenye bega langu la upande wa kushoto kwa uchovu aliyokuwa wa safari, sikuwa najua wapi pa kuelekea kwa usiku ule............... ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.