PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                         
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
  SEHEMU YA  22

   Ilipoishia sehemu ya ishirini na moja (21)................ Baada ya kushuka pale stendi, nilifuata konda na kumtaka atutolee mabegi yetu toka kwenye ile buti alimoyahifadhi. Nikiwa nimesimama kandoni mwa lile basi huku nimeshikila mabegi na Jenny akiwa ameniegemea kwenye bega langu la upande wa kushoto kwa uchovu aliyokuwa wa safari, sikuwa najua wapi pa kuelekea kwa usiku ule............... SASA ENDELEA

   Nilipata wazo la kumfuata konda kwa ajili ya kumuuliza kama atakuwa anajua kuwa sehemu gani tunaweza kupata nyumba ya wageni (guest), bila hiana yule konda alinielekeza kwenye nyumba ya wageni iliyopo karibu na pale stendi. Nilimwambia Jenny tuelekee sehemu hiyo niliyoelekezwa, nilibeba mabegi yetu tayari kufika mahali hapo.
   Tulienda moja kwa moja mpaka hapo kwenye hiyo nyumba ya wageni nilipoelekezwa kwa kufuata maelekezo kiufasaha zaidi. Tulipofika kabla ya kuingia ndani, alitokea muhudumu wa ile nyumba ya wageni na kunipokea begi moja "karibuni" (yule muhudumu alitukaribisha baada ya kunipokea begi na kuingia ndani)....
"asante dada" (Jenny aliipokea ile karibu ya yule muhudumu).
  Niliulizia bei ya chumba tukiwa bado tupo pale mapokezi, "bei ya chumba ni sh 10,000" (yule muhudumu alinijibu)....
"sawa" (nilikubaliana na yule muhudumu baada ya kujua bei ya chumba)....
"mnatakiwa kuandika majina yenu hapa kwenye daftari la wageni" (yule muhudumu alitutaka kuandika majina yetu kwenye daftari la wageni kwa ajili ya usalama wake na kutunza kumbukumbu ya wageni wanaoingia mahala pale)....
"poa, naitwa Ally Salim na mke wangu anaitwa Jamila Ally" (nilitaja majina ya uongo na Jenny alishindwa kuelewa kwanini nimefanya vile, yule muhudumu aliyaandika yale majina kwenye lile daftari la wageni pia alichukua ufunguo wa chumba na kutupeleka kwenye hicho chumba, alinisaidia kubeba begi moja tayari kuelekea hapo chumbani)....
"karibuni sana jamani" (yule muhudumu alitukaribisha tena kwa ukarimu wa hali ya juu)....
"asante dada" (niliikubari ile karibu yake yule muhudumu) "samahani dada, tunaweza kupata chakula?" (nilimuuliza yule muhudumu kama tunaweza kupata chakula kwa muda ule wakati alipokuwa anataka kutoka mle chumbani)....
"Ndio mtapata, chakula gani sijui?"....
"utakula nini mke wangu" (nilimuuliza Jenny)....
"chakula chochote kitakacho patikanika" (Jenny alinijibu huku akiwa amejilaza kitandani kwa uchovu aliyokuwa nao)....
"sawa!, naomba tuletee wali sahani mbili na maji makubwa mawili" (nilimkubalia Jenny na kumuomba yule muhudumu atuletee hicho chakula pamoja na maji baada ya kumpa hela sh 5000/= kwa ajili ya kununilia chakula), "nenda kaoge mke wangu kupunguza huo uchovu uliyokuwa nao" (nilimtaka Jenny akaoge baada ya yule muhudumu kutoka mle chumbani tayari kwenda kututafutia chakula).
  Baada ya muda mfupi kupita, Jenny akiwa bado yupo bafuni akioga nilisikia mlango wa chumba chetu ukigogwa, nikainuka tayari kwenda kufungua baada ya yule muhudumu kujitambulisha kuwa ndiyo yeye aliyekuwa anagonga mlango. 
  "Asante sana dada" (nilitoa shukrani yangu kwa yule muhudumu baada ya kupokea kile chakula alichokileta)....
"sawa" (yule muhudumu aliikubari shukrani yangu na kuondoka). Niliingia bafuni kwa ajili ya kuoga baada ya Jenny kutoka mle bafuni alipomaliza kuoga. 
  Kwa pamoja tulianza kula chakula baada ya mimi kutoka mle bafuni nilipomaliza kuoga. "Unajua pale sijakuelewa mme wangu"....
"hujanielewa nini?"....
"kwanini umeamua kutaja majina ya uongo?" (Jenny aliniuliza tukiwa tunaendelea kula).................. ITAENDELEA
   

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.