PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                             
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
 SEHEMU YA 23

    ilipoishia sehemu ya ishirini na mbili (22)....................   Kwa pamoja tulianza kula chakula baada ya mimi kutoka mle bafuni nilipomaliza kuoga. "Unajua pale sijakuelewa mme wangu"....
"hujanielewa nini?"....
"kwanini umeamua kutaja majina ya uongo?" (Jenny aliniuliza tukiwa tunaendelea kula).................. SASA ENDELEA

(Nilicheka kidogo baada ya kulisikia lile swali aliloniuliza Jenny)....
"sasa mbona unacheka?"....
"hapana mke wangu!, nimeamua tu kufanya vile kwa sababu ya kujiimalishia usalama wetu",....
"mmmmh, bado sijakuelewa mme wangu kuwa unamaanisha nini kusema hivyo"....
(nilinyamaza kidogo) "nasema hivyo kwa sababu, namjua vizuri sana mzee John, ni lazima atatutafuta"....
"sasa itakuaje kama tutaanza kutafutwa?" (Jenny aliniuliza akiwa na wasiwasi juu ya hilo)....
"usijali mke wangu, hiyo ndiyo sababu iliyonipelekea kubadilisha majina yetu ili watu wa huku watujue kwa majina hayo, na kuanzia leo utaitwa Jamila tu na mavazi yako yatakuwa ni baibui na hijabu ili kulilinda jina lako pamoja na kuificha sura yako kwa wakati wote, na mimi nitakuwa naitwa Ally na mavazi yangu ni kanzu na baraghashia" (Jenny, nilimpa maelekezo mazuri sana kuhusu sababu ya mimi kutaja majina ya uongo na jinsi ya kuishi mahala pale)....
(Jenny alicheka kidogo baada ya kusikia hivyo) "ila nimezoea sana kukuita Theo mme wangu, sasa nitawezaje kulifuta jina la Theo kwenye akili yangu na kuliingiza jina jipya?" (Jenny aliniuliza kwa utani)....
"inakubidi ulifute tu na kulisahau kabisa jina la Theo, mke wangu"....
"sawa, nitajitahidi mme wangu" (Jenny alikubaliana na mimi, alichukua maji na kuyanywa baada ya kumaliza kula)...
"sawa!"....
"Lakini kwanini umeamua kufanya haya yote mme wangu, unajua mpaka sasahivi nipo kwenye kiza kinene nikiwa sijui kitu chochote kilichosababisha mpaka tutoroke morogoro, naomba unitoe basi kwenye hiki kiza kinene mme wangu" (Jenny aliniomba nimwambie ukweli kuhusiana na kutoroka kwetu)....
"usijali mke wangu, kesho asubuhi nitakwambia" (nilimtuliza Jenny na kumtaka tulale na mambo mengine tutayaongea itakapofika asubuhi)
"hapana!, naomba uniambie sasahivi ya kesho anayajua mungu" (Jenny aling'ang'ania kwa kutaka nimwambia kwa wakati ule)....
"sawa, ngoja nikwambie mke wangu, (nilinyamaza kidogo), kwanza naomba unisamehe mke wangu kwa kutokukuambia ukweli juu ya mambo yaliyokuwa yanatokea ambayo yalikuwa yananiweka katika wakati mgumu sana, pia nilikuwa naogopa kukwambia ukweli kutona na hali yako mke wangu, niliogopa kukusababishia mpango wa mawazo, lakini pia licha ya mapenzi yetu kuyafanya kuwa ni siri sana pale nyumbani ila Baba alikuwa anajua kinachoendelea kati yetu".....
"nini" (Jenny alishtuka sana baada ya kusikia kuwa Baba alikuwa anajua kila kitu kutuhusu)....................... ITAENDELA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.