PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

                                                       
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI
By theostar

Kwa mawasiliano zaidi
0692-794942
0654-105503.
      SEHEMU YA 24

   Ilipoishia sehemu ya ishirini na tatu (23)................. "sawa, ngoja nikwambie mke wangu, (nilinyamaza kidogo), kwanza naomba unisamehe mke wangu kwa kutokukuambia ukweli juu ya mambo yaliyokuwa yanatokea ambayo yalikuwa yananiweka katika wakati mgumu sana, pia nilikuwa naogopa kukwambia ukweli kutona na hali yako mke wangu, niliogopa kukusababishia msongo wa mawazo, lakini pia licha ya mapenzi yetu kuyafanya kuwa ni siri sana pale nyumbani ila Baba alikuwa anajua kinachoendelea kati yetu".....
"nini" (Jenny alishtuka sana baada ya kusikia kuwa Baba alikuwa anajua kila kitu kutuhusu)....................... SASA ENDELEA

   "Ndiyo mke wangu, kwani kuna siku Baba aliniita kazini kwake na aliniuliza kuhusu mahusiano yetu, lakini mimi nilimkatalia kata kata kuwa hatuna mahusiano, kwahiyo jambo hilo lilikuwa likiniumiza sana kichwani mwangu kwa kufikiria zaidi jinsi ya kulitatua, lakini akili yangu ilifikia mwisho kabisa kwa kufikiria ndiyo maana nikaamua kufanya maamuzi magumu sana  ya kuondoka pale nyumbani na kuwa mbali napo kabisa" (nilimweleza Jenny  kwa kirefu zaidi ili aweze kunielewa vizuri kuwa nini nilichokuwa namaanisha kutaka kuondoka pale nyumbani kwa kutoroka)....
"sawa mme wangu, nimekusamehe japo haukuwa na sababu ya kuniomba msamaha kwani ulilokuwa unalifanya ni kwa ajili ya kulilinda penzi letu, namshukuru mungu kwa kunipatia mume mwenye ustahimilivu kama wewe, naamini kuwa ni kaburi pekee ndiyo litakalotutenganisha sasa, nakupenda sana mume wangu"....
"nakupenda pia mke wangu"....
"kwahiyo tutakaa mpaka lini hapa?"(Jenny aliniuliza kwa kutaka kujua kuwa tutaa kwa muda gani pale kwenye ile nyumba ya wageni)....
"mpaka tutakapopata chumba cha kupanga huko nje mke wangu"....
"sawa mume wangu, ila inatubidi tutafute haraka hicho chumba, maana gharama ya humu ndani ni kubwa sana" (Jenny alikuwa na hofu juu ya gharama ya pale kwenye ile nyumba ya wageni, kwani malipo yalikuwa yanafanyika kwa kila siku)....
"ni kweli mke wangu, ila usijali kwa hilo nitalifanyia kazi haraka iwezekanavyo"....
"sawa" (Jenny alikubaliana na mimi, story za hapa na pale ziliendelea tayari kuukaribisha usingizi uchukue na nafasi yake kwa usiku ule).
   Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni mzuri sana kwangu, kwani kuanzia niujue ujauzito wa Jenny pale nyumbani sijawahi kupata usingizi mnono kutokana na mawazo mengi yaliyokuwa yananisumbua juu yake dhidi ya wazazi.
    Majira ya saa 11 alfajili, nilishtuka kutoka usingizini baada ya jogoo wa kijijini kuwika, niliamka toka kitandani na kuingia chooni kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo, nilirudi kitandani baada ya kumaliza kujisaidia. Sikuweza tena kupata usingizi kwa wakati ule, kwani kulishaanza kupambazuka na miwiko ya jogoo tofauti tofauti pamoja na milio mizuri ya ndege wa angani vilichangia pia nishindwe kuupata usingizi alfajili ile, nilikaa pale kitandani nikiwa nafikiria jinsi ya kuyaendesha maisha ya pale kijijini, Jenny akiwa bado amelala ghafla alishtuka toka usingizini huku akiwa anahema kwa kasi ajabu.................... ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI

PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.