PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.
![]() |
| PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya ishirini na nne (24)........................ Sikuweza tena kupata usingizi kwa wakati ule, kwani kulishaanza kupambazuka na miwiko ya jogoo tofauti tofauti pamoja na milio mizuri ya ndege wa angani vilichangia pia nishindwe kuupata usingizi alfajili ile, nilikaa pale kitandani nikiwa nafikiria jinsi ya kuyaendesha maisha ya pale kijijini, Jenny akiwa bado amelala ghafla alishtuka toka usingizini huku akiwa anahema kwa kasi ajabu.................... ITAENDELEA
"Vipi mke wangu, mbona hivyo?" (nilimuuliza Jenny akiwa tayari ile hali yake imetulia kidogo)....
(Jenny hakuweza kunijibu chochote kwa muda ule)....
(nilikuwa kimya kwa dakika chache) "heti mke wangu?" (nilimuhimiza Jenny ili aweze kuniambia)....
(Jenny alikuwa kimya kwa dakika chache) "ni ndoto tu mme wangu" (Jenny alinijibu, hali yake ikiwa ametulia, kuwa ndoto ndiyo ilikuwa inasumbua)....
"mmmmh, ndoto!, ni ndoto ya aina gani hiyo mpaka ulikuwa unahema kiasi kile?" (nimuuliza Jenny kwa mshtuko mkubwa sana baada ya kusikia hivyo)....
"mmmmh, hapana, (alinyamaza kidogo), hapana haiwezi kutokea" (Jenny alionekana kuogopeshwa sana na hiyo ndoto)....
"sasa si uniambie mke wangu, mbona unaniweka kwenye wakati mgumu lakini?" (nilimtaka Jenny aniambie hiyo ndoto kuwa ni ndoto gani, kwani kwa wasiwasi aliyokuwa nao Jenny juu ya hiyo ndoto ulinifanya na mimi pia kuwa na wasiwasi)....
(Jenny alikuwa kimya kwa dakika chache) "ni wewe mme wangu"....
"eeeeeh!, mimi tena!, (nilishtuka sana baada ya kusikia kuwa hiyo ndoto ilikuwa inanihusu)....
"ndiyo"....
"mmmmh, kwahiyo imekuaje hiyo ndoto?"....
(Jenny alikuwa kimya kwa dakika chache) "umekamatwa na polisi na walikuwa wanakupiga sana mme wangu"....
"eheee, baada ya hapo?"....
"walikuburuza na kwenda kukupakia kwenye gari lao"....
"mmmmh, kwahiyo wewe ulikuwa na wasiwasi sana juu yangu?"....
"ndiyo mme wangu"....
"usijali mke wangu hiyo ni ndoto tu bwana, naamini kuwa haitotokea kwani mimi sina tabia ya wizi wala siyo mkorofi, sasa hao polisi watanikamatia wapi na kwa kosa gani?, kwahiyo wewe ipuuze tu hiyo ndoto haiwez kutokea kabisa" (nilimtoa Jenny wasiwasi aliokuwa nao kutokana na hiyo ndoto ya kutisha)....
"mmmmh, sawa mme wangu" (Jenny alikubaliana na mimi kishingo upande, alinyanyuka toka kitandani na kuingia chooni).
Asubuhi ya kwanza kwetu katika kijiji kile ilikuwa imekumbwa na msukosuko kidogo kutokana na ile ndoto, kwani Jenny alishindwa kuipuuza kabisa.
Baada ya siku nne, tulianza kuwa wenyeji katika kijiji kile, siku hiyo tukiwa tunakula chakula cha mchana kwenye mgahawa mmoja ambao ndiyo ulikuwa mgahawa wetu wa kupata chakula kwa wakati wote ndani ya siku hizo nne, nilijaribu kumuuliza yule mama ntilie kama anaweza kujua sehemu ambayo kunaweza kupatikanika chumba cha kupanga baada ya story za hapa na pale zilivyokolea zilinifanya niweze kuiingiza hio mada kiwepesi sana. "Kwani nyie mmetokea wapi na kwa sasa mnakaa wapi?" (yule mama ntilie aliniuliza baada ya kugusia habari ya chumba na alitaka kutufahamu zaidi)....
"sisi tumetoka Dodoma, na hapa tumefikia kwenye nyumba ya wageni iliyopo pale karibu na stendi, sasa gharama ya chumba pale ni ghari sana halafu bado tupo hapa kwa muda mrefu sana, (kwa makusudi nilimjibu yule mama ntilie kwa kumdanganya sehemu tuliotoka kwa sababu ya kujitengenezea mazingira mazuri pale kijijini)....
"kwahiyo hapa kijijini mna kazi gani?" (yule mama ntilie alihoji kwa undani zaidi akitaka kuijua kazi iliyotuweka pale kijijini)....
"bado hatuna kazi mama, kwani leo tuna siku ya nne hapa kijijini kuanzia tufike kwahiyo bado ni wageni sana"....
"sawa wanangu, lakini huku hakuna nyumba zenye vyumba vya kupangishwa"....
(nilivuta pumzi kwa kasi na kuiachia kwa kasi pia baada ya kusikia hivyo, kwani tulivyokuwa tunaendelea kukaa pale kwenye ile nyumba ya wageni ndiyo hela ilikuwa inatumika sana, na ukizingatia tulikuwa hatuna kazi yoyote ya kutuingizia hela)........................... ITAENDELEA

Comments
Post a Comment