PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI.
![]() |
PENZI LA MTOTO WA SHANGAZI By theostar Kwa mawasiliano zaidi 0692-794942 0654-105503. |
Ilipoishia sehemu ya thelathini na moja (31)................... Safari ya kwenda kwa yule mama tulioelekezwa na yule mama ntilie iliishia pale pale kwa yule mzee. Yule mzee alianza kututembeza katika eneo lake lililozunguka nyumba zake huku stori za hapa na pale zikiwa zinaendelea. "Sasa babu, tunaomba tukuache mara moja tu ili tukachukue kilichochetu pale kwenye nyumba ya wageni"....
"sawa vijana wangu" (yule mzee alikubaliana na mimi, tuliondoka na kumuacha mzee Jakob akiwa mwenye furaha sana, tulielekea moja kwa moja kule kwenye nyumba ya wageni tayari kwenda kuchukua kilichochetu ili kuhamishia makazi mapya kwa yule mzee).
Niliogopa sana baada ya kukalibia kufika kwenye ile nyumba ya wageni na kuwaona askari polisi waliokuwa wamebeba bunduki wakiwa wamejaa kwa kuizunguka ile nyumba ya wageni...................... SASA ENDELEA
"Mungu wangu" (Jenny alistaajabu kwa kulitaja jina la Mungu juu ya hofu kubwa sana aliyokuwa nayo baada ya kuwaona wale askari polisi katika mazingira yale ya nyumba ya wageni) "kwahiyo tunafanyaje" (Jenny aliniuliza huku akiwa bado mwenye hofu kubwa sana)....
"daaah, yani hapa hata sielewi nini cha kufanya" (nilimjibu hivyo Jenny kwani kwa muda huo nilishindwa kujua nini cha kufanya) "au twende kwanza kwa yule mama ntilie, tukakae pale halafu huku tuje badae kabisa"....
"sawa".
Safari ya kwenda kwenye ile nyumba ya wageni iliishia pale, tulianza safari mpya ya kwenda kwa mama ntilie "habari za sasahivi mama" (nilimjulia hali yule mama ntilie baada ya kufika pale)....
"safi!, habari za mtokako"....
"safi kabisa mama, tunashukuru sana tumepata sehemu japokuwa siyo hapo ulipotuelekeza"....
"sawa, mmepata wapi?"....
"kwa mzee mmoja hivi anaitwa Jakob"....
"mzee Jakob!, Ahaaaa yule mzee pale nyumbani kwake kuna mti"....
"ndiyo hapo hapo"....
"heeee, mmefikaje pale?" (yule mama ntilie alishangaa baada ya kusikia tumepata nyumba ya kuishi kwa huyo mzee Jakob, alitaka kujua kuwa tulifikaje)....
"ni story ndefu kidogo mama, ila kwa kifupi zaidi, tumefika pale kwa mipango ya mungu tu"....
"ahaaa, sawa!" (yule mama ntilie alikubaliana na mimi, tulibaki pale kwa muda mrefu kidogo tukiwa tunavizia muda sahihi wa kwenda kwenye ile nyumba ya wageni, story za hapa na pale zilichukua nafasi yake).
Baada ya masaa kadhaa kukatika tukiwa pale kwa mama ntilie, niliona tayari muda wa kukaa pale kwa mama ntilie umeisha, nilimuaga yule mama ntilie tayari kwa kuondoka, "tutaonana badae mama" (Jenny nae aliaga huku tukiwa tunatoka mle mgahawani)....
"sawa mwanangu".
Tulipofika pale kwenye nyumba ya wageni, tulimkuta muhudumu mwingine "habari yako dada" (nilimsalimia yule muhudumu)....
"safi kaka, karibuni"....
"asante, ila sisi ni wenyeji humu ndani tuna siku tano hivi, lakini leo tunatoka, sijue una taarifa yoyote juu yetu?"....
"hapana, kwasababu mimi nipo kwa dharula tu, kwahiyo sina taarifa yoyote juu yenu"....
"kwani yule dada aliyekuwa anatuhumia yuko wapi?" (nilimuuliza yule muhudumu mgeni kwa kutaka kujua kuwa nini kilichokuwa kinaendelea pale)....
"amechukuliwa na polisi, kwahiyo yupo huko kituoni"....
"mmmmh, kwani amefanya kosa gani?"....
"hapana yeye hana kosa lolote ila amechukuliwa tu kwa ajili ya kwenda kuhojiwa zaidi, kwani inasadikika kuwa aliwapokea majambazi sugu wawili"....
"ahaaa, kwahiyo unatusaidiaje ili tuchukue mizigo yetu"....
"mmmmh, kwani ipo chumba namba ngapi?" (yule muhudumu aliniuliza)....
"chumba namba 200"....
"majina yenu" (yule muhudumu alitaka kuyajua majina yetu)....
"Ally Abdala na Jamila Ally" (yule muhudumu alichukua taftari la wageni na kuanza kulipekua kutafuta majina yetu)....
"sawa, mna siku ya sita leo, mmelipia siku tano tu, siku ya leo bado hamjailipia, lakini pia mimi siwezi kuwakabidhi mizigo yenu bila taarifa maalum".......................... ITAENDELEA

Comments
Post a Comment