MALIPO YA USALITI
![]() |
MALIPO YA USALITI By Theostar Kwa mawasiliano zaidi 0673-779766 0782-589866 |
SEHEMU YA 2
Ilipoishia sehemu ya 1 "(Juma alimsindikiza Halieth kwa macho tu yaliyokuwa yamejawa na tamaa ya kutaka kumwona Halieth akiwa anatembea tu kwa jinsi anavyozichezesha nyama za makalio yake)"............... SASA ENDELEA
Majira ya saa mbili na dakika kumi na tano usiku (20:15) Juma aliwasili Suzy's restaurant sehemu ya makutano. Alipofika sehemu husika Juma alitoa simu kwenye mfuko wa suruali yake na kumpigia Halieth, Halieth alipokea simu iliyokuwa ikiita kwa namba mpya "hallow"...
"Halieth, unaongea na Juma! Habari yako" (Juma alianza mazungumzo kwa kujitambulisha kwa Halieth kwa sababu alitumia namba mpya)....
Mimi nipo salama, hofu kwako tu...
Mimi pia nipo salama...
Ni jambo la kumshukuru Mungu! Mimi nipo njiani naelekea mahala tulipokubariana kukutana ...
Sawa, mimi nimefika hapa muda mfupi...
Heeeeh! Nilijua kuwa nitafika kabla yako kumbe umeniwahi tayari (Halieth alishangaa baada ya kusikia kuwa Juma ameshawasili sehemu ya makutano yao mapema)...
Ndiyo...
Sawa, nafika hapo muda si mrefu...
Poa, nakusubiri! (Juma alikata simu na kuitia mfukoni mwa suruali yake huku akiingia ndani ya restaurant).
"Naomba juisi ya embe" (sauti ya Juma ilisikika ikiomba juisi ya embe kwa mhudumu wa restaurant ile baada ya kuketi mezani na mhudumu kuja kumsikiliza).
Mhudumu hakukawia kuipeleka juisi kwenye meza ya Juma, mziki mtamu uliokuwa ukiburudisha wateja wa restaurant ile uliifanya juisi iwe tamu mara dufu. Fikira za hapa na pale zilikua zikielea kwenye ubongo wa kichwa cha Juma zikitafakari wito wa Halieth usiku ule, nilishituliwa na simu ilivyokua inaita, nikaitoa mfukoni na kuipokea "niambie Halieth"...
Nimefika hapa, nataka niingie ndani, umekaa upande upi? (Halieth alimtaarifu Juma kuwa ameshafika na ametaka amjuze upande aliopo)...
Njoo hapa kwenye taa ya blue...
Poa! (Halieth alikata simu baada ya kujuzwa).
"Karibu!" (Juma alimkaribisha Halieth baada ya kufika mahala alipo)...
Asante! (Halieth alimshukuru Juma kwa kumkaribisha huku akikisogeza vizuri kitu tayari kwa kukaa)...
Vipi kazi zimeendaje? (Juma alimuuliza Halieth maendeleo ya kazi)...
Nashukuru Mungu zimeenda salama, sijui kwako?...
Kwangu pia zimeenda vizuri kwa msaada wa Mungu...
(Mhudumu alifika kwenye meza ya Juma kuwa mara nyingine) "karibu dada, nikuhudumie nini?" (Yule mhudumu alimuuliza Halieth)...
Naomba uniletee chipsi na kuku nusu...
Na mimi niletee kuku nusu pia niongeze juisi (Juma alidakia baada ya Halieth kutoa oda ya chakula anachokihitaji)...
Sawa! (Yule mhudumu alikubari kwa unyenyekevu kisha akaondoka kwenda kuwaandalia vyakula walivyovihitaji)...
(Kimya kilitanda kwa muda mfupi baada ya mhudumu kuondoka, kila mmoja akimtegea mwenzake aanzishe story)
"Ehee! Nakusikiliza Halieth" (Juma aliamua kuuvunja ukimya akimtaka Halieth aseme kitu juu ya mkutano ule)...
(Halieth akawa kimya kwa muda mfupi, alivuta pumzi kwa kasi na kuiachia taratibu) Juma! Nadhani unajua fika kwamba sisi wanawake tumenyimwa uhuru wa kuwa wa kwanza kujieleza juu ya hisia zetu kwa wanaume tuwapendao, lakini leo najipa mwenyewe uhuru wa kuwa wa kwanza kujieleza juu ya hisia zangu kwa mwanaume nimpendae kwa sababu nimechoka kusubiri kuambiwa. Sidhani kama nitakua nakosea kufanya hivyo...
Hapana! Hukosei kufanya vile moyo wako unataka Halieth, kwani ni nani anayezitesa hisia zako?...................ITAENDELEA
Comments
Post a Comment