MALIPO YA USALITI

MALIPO YA USALITI By Theostar Kwa mawasiliano zaidi 0673-779766 0782-589866 SEHEMU YA 2 Ilipoishia sehemu ya 1 " (Juma alimsindikiza Halieth kwa macho tu yaliyokuwa yamejawa na tamaa ya kutaka kumwona Halieth akiwa anatembea tu kwa jinsi anavyozichezesha nyama za makalio yake)"............... SASA ENDELEA Majira ya saa mbili na dakika kumi na tano usiku (20:15) Juma aliwasili Suzy's restaurant sehemu ya makutano. Alipofika sehemu husika Juma alitoa simu kwenye mfuko wa suruali yake na kumpigia Halieth, Halieth alipokea simu iliyokuwa ikiita kwa namba mpya "hallow"... "Halieth, unaongea na Juma! Habari yako" (Juma alianza mazungumzo kwa kujitambulisha kwa Halieth kwa sababu alitumia namba mpya).... Mimi nipo salama, hofu kwako tu... Mimi pia nipo salama... Ni jambo la kumshukuru Mungu! Mimi nipo njiani naelekea mahala tu...